Adeladius Makwega-Musoma MARA
Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi amesema kuwa hakuna taifa ulimwenguni lililoendelea huku likiwaacha nyuma wafanyakazi wake, maendeleo ya taifa yanakwenda sambamba na begabega yakikokotana na Wafanyakazi lakini wafanyakazi wasijihusishe na ubadhilifu wa fedha zinazotolewa na Serikali na wafadhili katika miradi ya maendeleo.
“Serikali itaendelea kuwa makini na kuisimamia miradi hiyo lakini wafanyakazi wabadilifu serikali haitovumilia.”
Haya yamesemwa na Kanali Mtambi katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi mkoani Mara Mei Mosi 2025 mbele ya maelfu ya wafanyakazi katika viwanja vya Mkendo.
“Serikali ililipa madeni ya wafanyakazi kwa wanatumishi wa Serikali za Mitaa na Serikali Kuu huku serikali ikiwapandisha madaraja watumisihi kadhaa na kutoa ajira zinazokaribia 1700 kwa mkoa wa Mara pekee kazi yote hii imefanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”
Kanali Mtambi aliongeza kuwa kumefanyika vikao vya mabaraza ya wafanyakazi, huku akiwataka wajiri wote wakumbuke majukumu yao mathalani kupeleka pesa za watumishi katika mifuko ya hifadhi na hata kupeleka fedha katika mifuko ya fidia ili kusaidia watumishi kulipwa stahiki hizi pale wanapopatwa na changamoto kazini, stahiki za wafanyakazi zilipwe kwa wakati na hili litaepusha kulimbikizwa madeni.
Kanali Mtambi aliongeza kuwa siku hii inaambatana na kutoa zawadi kwa wafanyakazi bora huku akiwapongeza wafanyakazi hodari huku akiwaomba wasibweteke kwa kupata zawadi hizo bali waongeze juhudi na wale waliokosa zaidi leo hii juhudi zao zitazaa matunda mbeleni.Awali kabla ya Mkuu wa Mkoa kuongea na Wafanyakazi hao risala ya wafanyakazi hao ilizitaja changamoto kadhaa.
Kabla ya kuanza shughuli hii Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alikagua mabanda mbalimbali ya shughuli zinazotoa huduma katika mkoa wake wake, mojawapo ya mabanda haya lilikuwa ni banda la TANESCO ambapo walielezea juu ya Jiko lao la umeme jipya ambalo linatumia uniti moja ya umeme kupikia maharage.
“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Jiko hili ni msaada mkubwa kwa watumiaji wa Umeme Mekoni , linatoa uhakiki wa matumizi ya umeme mdongo kwa wateja wetu, sasa wateja wasiwe na hofu , matumizi ya umeme kwa mapishi ni bora na mapishi yake ni bila moshi.”
Maelezo haya ya TANESCO yalitolewa mbele ya Kanali Mtambi na Bi Sarah Lukas Ndanga ambaye ni mhasibu msaidizi Shirika hili la Umma nchini Tanzania.
Kwa mkoa wa Mara Sherehe hii ilihudhuriliwa wafanyakazi kutoka vyama vyao kadhaa wakiwa na viongozi wao pamoja na wakuu wa taasisi binafsi na za umma, Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Wilayani, Makatibu Tawala wote wa Wilaya na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara ndugu Gerald Kusaya ambapo alipokuwa akimkaribisha Mkuu wa Mkoa alisema kuwa shughuli hii imeandaliwa ili wafanyakazi washerekee sikukuu yao akiwaomba wafanyakazi wafanye kazi wa heshima ya nafasi zao na kuonesha weledi kazini kwa kila jukumu wanalopewa katika wakiwa katika utumishi.
Historia ya Siku ya wafanyakazi dunia huadhimishwa kila Mei Mosi ya kila Mwaka kukumbuka hatua , madhila na balaa kadhaa walizopitiwa wafanyakazi duniani katika kudai haki zao za kufanya kazi, kufanya kazi saa nane kwa siku, malipo ya mishahara ya haki, mazingira bora na salama ya kazi na pia kupata muda na uhuru wa kuabudu siku moja ya juma.
0717649257
Post a Comment