RAIS SAMIA MWANA USHIRIKA NAMBA MOJA-KANALI MTAMBI

 


Adeladius Makwega-Musoma MARA

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi amesema , Wanaushirika wanapaswa kuwa wabunifu, ili kujenga Ushirika Imara katika sekta za Uvuvi, Ufugaji , Uchimbaji wa Madini na fursa zingine ili kukuza uchumi wa Mkoa wa Mara na Taifa zima la Tanzania maana Ushirika ni Falsafa wa Mwana Mara, Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere huku Rais Samia ni Mwana Ushirika Namba Moja.

“Lazima wana ushirika waimarishe mfumo wa stakabadhi gharani maana mfumo huu unaonekana kuwa na tija sana mathalani zao la Choroko bei ya mtaani ilikuwa shilingi 700-1000 lakini baada ya Stakabadhi gharani bei imekuwa hadi shilingi 1410 hii inakaribia mara moja zaidi. Wana ushirika muingie katika mfumo huu ili mpate bei kubwa ya mazao yenu huku ikifanya shughuli zenu na mifumo bora ya TEHAMA mathalani hadi Mei 30, 2025 vyama vyote vimejiunga katika mfumo wa TEHAMA ili muende na wakati.”

Haya yamesemwa Mei 8, 2025 katika uzinduzi wa Kongamano la Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Mara lenye kauli mbiu kuwa Ushirika ni Biashara. Akizungumza kwa msisitizo mkubwa Kanali Mtambi alisema anatambu changamoto kadhaa zilizopo katika Ushirika mathalani uhujumu uchumi na Serikali ya Mkoa wa Mara haitolivumilia hili. Huku akiagiza Wakuu wa Wilaya zote hapa Mara kuzitatua changamoto zilizopo katika Ushirika wilayani mwao.

“Kongamano hili liwe fursa thabiti ya kutoa maoni, ushauri na mchango wenu wa mawazo katika Ushirika wetu, muwe huru na Serikali ya Mkoa wa Mara itayafanyia kazi maoni yenu.”

Mwishoni Kanali Mtambi aliwashukuru sana wana wa Ushirika kwa kumchagua yeye kuwa Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo akisema kuwa anakumbuka kuwa Kongomano la mwaka jana 2024 pia alikuwa Mgeni Rasmi na anaona kuwa hali ya Ushirika ya mwaka 2024 hailingani na ya mwaka wa 2025 Ushirika Mkoani Mara umekuwa bora zaidi. Awali akisoma risala wa Wanaushirika Mkoa wa Mara Katibu wa Wanaushirika huo ndugu Samweli Kissobove alimwambia Mkuu wa Mkoa Mara kuwa,

“Mkoa wa Mara una wanaushirika wenye uwekezaji mkubwa katika Nyanja mbalimbali ikiwamo zaidi ya Bilioni 28 katika viwanda vya kuchakata kahawa na hata biashara nyingine.”

Wakiwa na kipaumbele cha kuwekeza mitaji yao katika uwekezaji mkubwa zaidi, lakini kwa sasa kinachofanyika ni kutambua rasilimali zote walizonazo kisha kuzitambua ili wanapofanya uwekezaji basi wanatambua wana nini na wanafanya uwekezaji wao wapi?

“Ushirikia umewekeza karibu bilioni 15.1 katika ununuzi wa mazao kadhaa kama vile pamba na hilo limesaidia kuwanufaisha wakulima na Ushirika kupata faida ya kutosha na kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi kwa Mkoa wa Mara.”

Katika ufunguzi wa Kongomano hili ilielezwa kuwa mfumo wa Stakabadhi Gharani katika zao la Choroko umefanyika kupitia ushirikia na huku minada miwili imefanyika katika Halmashauri ya Bunda Mji, Bunda Vijijini na Musoma Vijijini huku wakiwa na malengo ya kuongeza nguvu zaidi katika zao la Ndegu.

“Awali bei ya Ndengu na Choroko ilikuwa chini lakini baada ya mfumo wa Stakabadhi Gharani umesaidia wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya juu zaidi.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wanaushirika Mkoa wa Mara alisema kuwa Jukwaa lao linasaidia mno wana wa Ushirika kufahamia na kueleza changamoto zao na kujibiwa maswali waliyo nayo naye


 

Katibu wa Ushirika Mkoa wa Mara ndugu Kissibove alisema kuwa wana mitaji midogo ambapo inazorotesha uwekezaji mkubwa na kuzipata fursa kubwa zaidi, upungufu wa rasilimali fedha na kuathiri uwekezaji na hata kudumaza uwekezaji huo na nyingine ikiwa vyombo vya uchunguzi kutumia muda mrefu kutatua baadhi ya mashauri mbele yao.  Shughuli hii imehudhuriwa na viongozi kadhaa wa Ushirika Mkoa mzima wa Mara Wakurugenzi Watendaji, Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya, Makatibu Tawala wote, na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara.

makwadeladius@gmail.com

0717649257





 

 

0/Post a Comment/Comments