
Adeladius Makwega-MBAGALA
“Nakwambia, katika kila mkoa tulichaguliwa waandishi wa habari watano watano na tuliambiwa kuwa mara baada ya zoezi la tathimini ya mali za chama waandishi hao watano watano kila mkoa tungepata ajira ya kudumu.”
Ndugu huyu aliendelea kusimulia kwa uchungu kuwa utaratibu wa awali ulikuwa kila mmoja wetu aliandika habari/ makala na kuitumia katika chombo chetu na mwisho wa siku kila mmoja alilipwa malipo ya habari/ makala aliyoiandika tu, tukawa tunafanya kazi kwa moyo wote na Mungu Bahati Marehemu John Pombe Magufuli mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa alipomaliza zoezi la uhakiki wa mali za chama akatufanyia jambo moja zuri ambalo lilikuwa SURPRISE kwetu.
“Kila mwandishi kati ya wale watano watano kila mkoa akapewa ofa ya kiwanja Jijini Dodoma na kila mwandishi alipewa karatasi yake ya ofa ya kiwanja hicho.”
Ndugu huyu anaendelea kusimulia kuwa moyo wa kazi ulikuwa maradufu lakini shetani hana adabu kabisa, kwa Bahati Mbaya Magufuli akafariki dunia, wale tulioweza kwenda kuzika tulifanya hivyo na wale walikuwa hawana nauli au kukosa gari za kudoea lifti wakabaki makwao, huku wakimuomba dua Mwenyezi Mungu amrehemu na kumsamehe dhambi zake. Tanzania ikapata Rais Mpya Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye alikuwa Makamu Rais wa Dkt. John Pombe Magufuli awali.
Mama Samia akaanza na uongozi wake vizuri tu, mwanzoni, mwanzoni tu mama akajikwaa kukubali kuhojiwa na Chombo Kimoja cha Kimataifa, majibu ya mama yakaleta shida baada ya kuandikwa habari juu ya Mama Hatogombea 2025 wanahabrai walimnukuu kimakosa, choko choko ikiwa mahojiano hayo hayo.Hilo likaleta shida mara akina SUNGURA wakaondolewa.
“Wale akina SUNGURA walikuwa wakifanya kazi nzuri, walikuwa na uwezo mkubwa, makosa yapo katika Uandishi wa Habari hata NEW YORK TIMES likitoka lazima kuna kuwa makosa na kesho yake mnakaa mnafanya POSTMORTEM kuyarekebisha, lakini haikuwa hivyo, waliondolewa na gazeti kufungiwa siku dazeni moja na ushehe.”
Ndugu huyu anaongea kwa uchungu mno,
“Wale akina SUNGURA walikuwa watu sahihi lakini hawa waliopa sasa hawawezi kuifanya kazi hiyo vizuri, magazeti yetu sasa anasoma nani?Je Magazeti ya chama chetu yataweza kufanya kazi kwa faida? Lazima tufanye kazi kibiashara na huku tukifanya propaganda ya chama hiki kwa Ueledi. Makosa yapo na likitokea kosa tunakaa tunazungumza maana sisi sote ni CCM. Hivi kila mtu Mungu akaamua kumuonesha Video ya Makosa yake yupo ambaye atakuwa salama? Magazeti ni yetu,chama ni chetu, sasa kama CCM tunafukuzana tutakuwa wageni wa nani? Ukienda huku unaambiwa hili ni LISISIEMU.T utakuwa wageni wa nani jamani?Tunakimbilia wapi?”
Ndugu huyu alisema kuwa suala la mwanachama wetu kugombea au kutogombea haliwezi kutugombanisha wenyewe kwa wenyewe kama si wewe ni mwanachama mwingine wa CCM maana sisi sote ni Chama Cha Mapinduzi(CCM) hapa hekima ya haki ingetumika akina SUNGURA wangebaki na kwa hakika sasa na magazeti yetu tungekuwa mbali.
“Suala la Gazeti la uhuru pia linatoa picha hata namna chama na serikali yetu mahusiano yake na vyombo vya habari kila linapotokea shida, shida kwa binadamu zipo kikubwa ni namna tunavyotatua shida hizo tu ”
Ndugu huyu anasema kuwa zile ajira tano kwa wanahabari wa kila mkoa mpaka kesho hilo halikutimia na hata zile ofa zao za viwanja Jijini Dodoma wamebaki na makaratasi, hata ukiuliza Jijini wanajibiwa kuwa viwanja hivyo wamepewa watu wengine.
“Sisi tumebaki na makaratasi ya Ofa za vile viwanja tu.”
Ndugu huyu alimalizia kusema kuwa yaani mie mwanaCCM ninakuwa kama Mpinzani vile!
Je upinzani ukija kuchukua nchi si nitakuwa na hali mbaya zaidi, maana kila mmoja anajua mie mwanaCCM, mazungumzo haya yaliendelea kwa muda iasha yalikatishwa na wimbo wenye maneno haya mkutanoni.
“Inang’ara CCM, Kimenuka kwa Wapinzani…”
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Ni kweli kabisa inawezekana Gazeti Letu la Uhuru lilifanya kosa ambalo kihabari POSTMORTEM ya siku iliyofuata ilitosha kutambua kilichotokea na kuomba radhi. Kwa hakika Gazeti la Uhuru halikupaswa kufungiwa siku zile dazeni moja na ushehe.
“Kwa hali ilivyo sasa, sisi WanaCCM wenyewe kwa wenyewe tunafanyiana hivi? Je wapinzani wakija kuchukua nchi itakuwaje? Hatuna pa kukimbilia jamani.”
Haya ni malalamiko ya Mwana CCM mwenyewe na haya malalamiko ilitakiwa yaandikwe kama makala katika MAGAZETI yetu la CHAMA CHA MAPINDUZI ya Uhuru na Mzalendo,chama chetu lakini ,lakini ,lakini wahariri wa sasa wanacho kifua hicho? hawaogopi yaliyomkuta SUNGURA?Hata kama yakifika mezani kwao hawawezi kuandika haya, kumbuka walalamikaji ni wanachama wa CCM.
Mwanakwetu kwa makala haya anamuomba Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi, Dkt. Emmanuel Nchimbi ajitahidi mno kuyafanyia kazi malalamiko haya ya wana CCM kabla ajamkabidhi mtu mwingine nafasi hiyo.
“Kutoa ajira tano tano kwa wana habari watano watano kila mkoa na pia zile ofa za viwanja walizopewa na Mwenyekiti wao wa wakati huo marehemu John Pombe Magufuli.Hata lile suala la waliondolewa kwenye magazeti yetu lifanyiwa kazi.”
Hili linatoa taswira je viongozi wakubwa wa CCM wanakaaje na waandishi habari katika vyombo vyao?Je hali inakuwaje mahusiano ya CCM na waandishi wa habari wengine wasio chini ya CCM?CCM LAZIMA IWE MFANO WA WAAJIRI WOTE MAANA NDICHO CHAMA DOLA.
Mwanakwetu anamalizia makala haya kwa ubeti huu wa shairi hili la TANU,
Chama ni Chombo Muhimu
Tukifanye cha Kudumu
Tusije kutia Sumu
Kwa Tamaa ziso Njia.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya niyaitaje?
Jamani Tutakimbilia Wapi? Au Hawawezi ,Wanaogopa Kumfuata Sungura. Mwanakwetu anachagua Hawawezi Wanaogopa Kumfuta SUNGURA.
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
NB;1. Makala haya yameandikwa kwa heshima na Binamu wa Mwanakwetu anayefahamika kama Mwalimu Msekwa Njama anayesomesha Sekondari Jijini Dodoma.
2. Ubeti wa shairi hili lililotumika
unatoka Utenzi wa Kumbukumbu za Azimo La
Arusha -G A Mhina ukurasa 13 ubeti 190., Mchapaji ni Black Star Agencies PO
Box 3978 Dar es Salaam Tanzania
Post a Comment