WEWE MCHINA MWEUSI

Adeladius Makwega Tarime  MARA

Msomaji wangu kumbuka Mwanakwetu bado yu Wilaya Tarime ambayo inaongoza na Meja Edward Gowele, hii ni wilaya mojawapo kati ya 9 za Mkoa wa Mara. Zamani ilijulikana kwa jina la

"Wilaya ya Mara Kaskazini."

Jina Mara linatoka na Mto Mara ambapo mto huu upo Kenya naTanzania. Beseni lake ni la km2 13,504, ambazo 65% ziko Kenya na 35% zipo Tanzania ukimwanga maji yake Ziwa Victoria.

Mwaka 2006 sehemu ya mashariki ya Tarime ikawa wilaya mpya ya Rorya. Tarime imepakana na Kenya (kaunti za Migori, Trans Mara na Kisii) upande wa kaskazini na mashariki. Hifadhi ya wanyama ya Masai Mara ya Kenya uko upande wa mashariki pia. Upande wa kusini imepakana na wilaya za Musoma mjini, Musoma vijijini na wilaya ya Serengeti. Upande wa magharibi iko wilaya mpya ya Rorya. 


 

Kumbuka Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi yu Wilayani Tarime akikagua miradi ya maendeleo na sasa anatoka Shule ya Sekondari Julius Kambarage Nyerere akielekea kuzungumza na Wakandarasi Wazawa.

Safari hii ilikuwa ya mwendo kidogo kisha kufika katika eneo ambapo kulikuwa na Ofisi ya kampuni moja inayojulikana RIN.

Hapa Mkuu wa Mkoa alipokelewa na mwenyeji wake  Meja Gowele.

“Hii kampuni inashirikiana na sisi kwa kazi nyingi za maendeleo na ndiyo maana tumeona ni vizuri uitembelee uione namna inavyofanya kazi, karibu sana Mh. Mkuu wa Mkoa.”

Karibu na kijiji cha Nyamongo katika kata ya Nyamwaga kuna migodi ya dhahabu ya North Mara Gold Mine inayomilikiwa na kampuni Acacia Mining kutoka Uingereza na hii ni Kuwepo kandokando kwa utajiri mkubwa wa dhahabu.


 

Tukiwa hapa kiongozi wa Kampuni ya Rin alijitambusha na kueleza kazi zake alizofanya mpaka sasa; .

“Jina langu ni Isack Charles Lange ni Mkurugenzi wa kampuni hii,  tunafanya kazi za usafirishaji na ujenzi, tumeajili wafanykazi 300. Huku tukijitolea misaada mingi kwa watu binafsi na taasisi zako za umma.”

Mara baada ya Isack Lange kueleza mchango wake kwa jamii ya Wilaya ya Tarime na mkoa wa Mara ,Mkuu wa Mkoa wa Mara alianza kwa pongezi kwa kampuni hii.

“Kama umeajili vijana 300 wewe ni mchina mweusi huyu ni mchina mweusi .”

Historia ya Wilaya ya Tarime inadokeza kuwa Mwaka 1972 zilipoanzishwa Serikali za Mitaa, Wilaya ya Tarime ilikuwa na Tarafa 8, Kata 30, Vijiji 95 vitongoji 405 na Jimbo 1 (Tarime) la uchaguzi.


 

Miongoni mwa kata hizo ni

Binagi * Bumera * Ganyange * Gorong'a * Gwitiryo * Itiryo * Kemambo * Kibasuka * Kiore * Komaswa * Kwihancha * Manga * Matongo * Mbogi * Muriba * Mwema * Nyakonga * Nyamwaga * Nyansincha * Nyanungu * Nyarero * Nyarokoba * Pemba * Regicheri * Sirari  na Susuni

Baada ya mazungumzo haya Mkuu wa Mkoa wa Mara alishika usukani wa kikao hicho.

“Nimeweka mkakati kuwanyanyua wazabuni na Wakandarasi wazawa, hapa tutakuwa tunawafikia katika kila ziara zangu lakini ninachowaomba mkipewa kazi mzifanye vizuri.

Mara baada ya maelezo haya ya Mkuu wa mkoa wa Mara Kanali Mtambi msafara huo ulitoa nanga na kuanza safari ya kurudi Musoma Mjini

Kwa hakika msomaji wangu hivyo ndivyo ilivyokuwa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika Wilaya ya Tarime.


 

Mwanakwetu upo?

Kumbuka

"Wewe ni Mchina Mweusi.”

Nakutakia Siku njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257


















 

 

 



0/Post a Comment/Comments