Adeladius Makwega-MBAGALA
Msomaji wangu nakualika tena katika makala ya katuni siku ya leo, kumbuka haya ni makala ya uchambuzi wa katuni kama zilivyochorwa na kuzingatiwa na wachoraji wa katuni hizo kutoka vyanzo mbalimbali.
Kuyaanza makala haya siku ya leo ninaikamata katuni ya kwanza ambayo inawaonesha jamaa wapo uwanjani wakicheza mpira wa miguu na kuna timu imevaa jezi ya rangi za kijani na kuna timu nyingine wamevaa jesi za rangi na bluu na nyekundu, ukitazama wachezai wenye kijani yupo mchezaji mmoja mwanamke mwwnye mavazi na sura inayoshabiana na Samia Suluhu Hassan. Nako upande wa pili yupo mchezaji anayefanana na Tundu Lissu wa CHADEMA.
Nyuma ya Tundu Lissu midundo ya polisi imemvuta fulana machezaji huyu huku wakisema anaweza kufanya mchezo usinoge.
Huyu mchezaji mwenye sura kama ya Samia Suluhu Hassan akisema sasa tuendeleee taratibu taratibu hata wakisusa basi. Kwa hakika katuni hii inazumngumzia taifa za Tanzania mara baada ya Tundu Lissu kukamatwa na kuwekwa korokoroni hivi punde.
Mchoroja wa katuni hii Said wa Michael na Shirika lake la Utangazi Ulimwenguni DW wakiipaza sauti kupinga matumizi ya vyombo vya ulinzi kuwazuia wapinzani kushiriki vizuri siasa nchini Tanzania. Saidi wa Michael na Shirika la Utangazaji la Ujerumani kwa pamoja wakivisonta vidole vyombo hivyo vya ulinzi viache mara moja mambo haya .
Sasa Mwanakwetu anaikamata katuni ya pili ambayo imechorwa na Alwatan Masoud Kipanya ambapo kunaoneka kitu kama kontena limedondokea jamaa mmoja na kumfunika kabisa, Mungu bahati huyu jamaa, miguu yake iliyovaa viatu inaoneka vizuri na Kiganja cha mkono wa kuume kikioneka.
Katuni hii inaonesha kuwa kama Konrtena hilo lingaliweza kumdondokea na kumficha kabisa jamaa huyu ingekuwa hatari mno, maana asingaliweza hata kutambuliwa kwa hiyo Kontena hilo kubwa limeshindwa kukamilisha nia yake ya kumuangamiza kabisa ndugu huyu lakini sasa bado anaonekana .
Katuni hii ukiitazama vizuri na kwa umakini mkubwa inadokeza juu ya kukamatwa kwa Tundu Lissu mwanasiasa wa CHADEMA akiwa na mzigo huujuu yake wa tuhuma za uhaini mahakamani.
Tuhuma za uhaini ndilo ule mdondokeo wa Kontena lakini kontena lingemsagasaga ilikuwa hoja nzito lakini matumaini ni kwa Tundu Lissu anakuwa kama nyoka mwenye vichwa viwili, naye mchoraji wa Katuni hii bado anamatumaini ya Tundu Lissu kurejea tena katika ulingo wa siasa za Tanzania.
Mwandishi wa makala haya anatambua kuwa kama Tundu Lissu atatiwa hatiani kwa tuhuma hizo hukumu yake ni kifo.
“Mchoraji wa Katuni hii anayaibua matumaini makubwa kuwa ni vigumu kontena hilo kumpa madhara yoyote Kiongozi huyu wa upinzani nchini Tanzania na kwa sasa kumkamata Tundu Lissu ni mzigo mzito kwa vyombo vya ulinzi vya Tanzania ambayo vina deni kubwa la kuiambia jamii ya Watanzania nani alishiriki kumshambulia kwa risasi mwaka 2017. ”
Mwanakwetu anaikamata katuni ya tatu ambapo kunaonekana viatu vya mwanajeshi vilivyopewa maneno Abeid Karume mwaka 1905-1972 ambaye ndiye Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi anafariki dunia mwaka 1972.
Kwa kando kunaonekana Rais wa sasa wa Zanzibar na kando wapo jamaa kadhaa waliyoingoza Zanzibar baada ya Abeid Karume na midundo hii wote haiwatoshi.
Mchoraji wa katuni hii anaibua wazo lake kuwa mara baada ya kifo cha Abeid Karume viongozi wote waliyofuata wameshindwa kuvivaa viatu vya Sheikh Abeid Karume.
Mwaanakwetu anaikamata sasa katuni ya nne inayomuonesha jamaa mmoja anayefanana na Rais wa Marekani Donald Trump aliyevalia suti maridadi yenye bendera ya Marekani begani.
Bwana Mkubwa huyu ameipokonya Kamera kutoka kwa mwanahabari mmoja aliyepewa kibandiko VOA, jamaa aliyepokonywa Kamera anasema hili linatokea kwa mara ya kwanza baada ya miaka 83.Huku Donald Trump akisema mtanielewa tu.
Katuni hii imechorwa na Said wa Michael wa Shirika la Utangazaji la Ujerumani ikieleza namna Rais Donald Trump kupiga stopu urushwaji wa matangazo wa Shirika la Utangazaji la Propaganda la Marekani VOA kw akulipunguzia bajeti likimaanisha matangazo haya yaende likizo.
Kwa hakika katuni hii inamkumbusha Mwanakwetu kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea katika taifa la Ugiriki kwa kulifunga Shirika lake la Utangazaji lengo ni kubana matumizi.
Wahariri wa Shirika la Utangazaji la Ujerumani DW walilaumu sana Ugiriki kufikia hatua hii, wakirusha maneno kuwa taifa kama Ugiriki chimbuko la demkorasi haikuwa sahihi kulifunga shirika hilo. Bali Ugiriki lingelifanyia maboresho tu shirika lake la utangazaji.
Huku wahariri wa Ujerumani wkaisema kuwa kufungia Shirika la Utangazaji la taifa kunakofanywa na taifa lolote lile ni kosa kubwa maana serikali inakwepa jukumu lake na kuwapa taarifa raia wake na uhuru wa vyombo vya habari.
Mwanakwetu analitazama jambo hili la umakini mkubwa kwa vyombo vyote vya serikali barani Afrika vinatakiwa kufanya kazi kwa ushindani na ueledi ili kuepusha lawama na kupoteza watazamaji, wasikilizaji na wasomaje vinginevyo watajisoma wenyewe, kujisikiliza wenyewe na kujitazama wenyewer na lawama zozote dhidi yao ni hatari mwisho wa siku mashirika haya yatafungwa.
Maamuzi ya Rais wa Marekani na yale ya Ugiriki mwaka wa 2013 yanaweza kulikumba Tanzania hasa kwa TBC na TSN, kwa sasa wanajiendesha kwa faida? Je Kwa sasa wanawasomaji? Wana watazamaji Wana /wasikilizaji wangapi?
Mbona taasisi zingine binafsi zanajiendesha zenyewe na kulipa mishahara zenyewe lakini TBC na TSN mishahara inalipwa na Serikali ?
Je wasomaji/wasikilizaji/ watazamaji wake wanaongezeka? Je jamii ya Watanzania zinavitazamaji vyombo hivyo?Vyombo hivyo vimejawa na habari zisizo mizani na usawa ?
Kwa sasa ni lazima wanaongoza vyombo hivyo(TBC&TSN) wawe wabunifu, wafanye kazi kwa faida na kinyume chake muda si mrefu haya haya ya Ugiriki na Marekani yanaweza kutokea nchini Tanzania maana wanaolipa kodi ndiyo wanaolalamika kuwa vimeshindwa kutimiza malengo yake ya kuanzishwa.
Mwanakwetu upo?
Basi hadi hapo ndiyo Mwanakwetu anashusha nanga katika makala ya katuni siku ya leo, kumbuka siku ya leo makala haya yamjengwa katika katuni nne; ile ya mchezo wa soka baina ya CHADEMA na CCM ya pili ni ile ya Kontena lililomuangukia TUNDU LISSU, katuni ya tatu ni ya viatu vya Abeid Karume vilivyokosa mvaaji na katuni ya nne na mwisho ni hii VOA kupigwa stopu
Basi kwa katuni hizo ndiyo na mimi nakuaga katika makala ya katuni siku ya leo.
Kumbuka
“TBC TSN wajifunze Kwa VOA.”
Nakutakia siku njema
0717649257
Post a Comment