Adeladius Makwega-Musoma MARA
Aprili 23, 2025 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Balozi. Dkt. Emmanuel Nchimbi amefanya ziara ya kukagua miradi miwili mikubwa inayofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Mkoani Mara, ukiwemo Ujenzi wa Uwanja wa Ndege hapa Musoma Mjini na Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa ambayo ujenzi wake ulianza tangu wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere.
Kabla ya yote Katibu Mkuu Balozi Dkt. Nchimbi alikaribishwa na sala na dua kutika kwa viongozi wa dini ili kuipa baraka ziara yake hapa Musoma Mjini.
Kisha Mkuu wa Mkoa wa Mara kuyasema haya.
“Uwanja huu ni muhimu kwa Mkoa huu na hata upande huu wa Mashariki wa Ziwa Victoria.”
Haya yakiwa maelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ya Kanali Evans Alfred Mtambi ya awali mbele ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, mapema kabla ya haya Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mjini mhe. Jumaa Chikoka aliupokea ugeni huo wa Katibu Mkuu CCM Taifa hapa uwanjani kwa neno la ukaribisho na kisha Mbunge wa Musoma Mjini mhe.Vedastus Mathayo Manyinyi nayeye kutoa maelezo yake hapa hapa uwanjani;
“Ndugu Katibu Mkuu, pamoja na viongozi wote, hapa ni Uwanja wa Ndege wa Musoma, huu ndiyo Uwanja wa Ndege wa Musoma na Serikali imesikia kilio cha watu wa Musoma, kilichobaki ni jengo la wasafiri na kuna nyumba bado hazijalipwa fidia yake, naamini leo hii kilio chetu kitakwisha, wananchi wanadai bilioni tano na ushehe, tunaomba fidia ilipwe na jengo la wasafiri lijengwe haraka, uwanja huu utakuza uchumi wa watu wa Musoma na utasaidia hata kubeba watalii wafike Mbugani Serengeti maana kutoka Musoma hadi mbugani Serengeti ni KM 70 tu, nina hakika ndege nyingi za watalii zitatua hapa.”
Baadaye Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alimnyanyua Meneja wa TANROAD mkoa wa Mara ndugu Vedastus Maribe,
“Kiwanja hiki ujenzi wake unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kiwanja hiki zamani kilikuwa cha changarawe lakini sasa kitakuwa cha lami. huku kikitanuliwa na kuwezesha ndege kubwa zaidi kuruka na kutoa hapa kuliko kama ilivyokuwa awali. Mradi huu umefikia asilimia 58 na utakamilika mapema Septemba 2025.”
Katibu Mkuu Balozi, Dkt Emmanauel Nchimbi alikagua Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Musoma Kisha kusema neno,
“Uwanja wa Ndege wa Musoma utasaidia utalii kuimarika, nashukuru mita 1000 lami zimekamilika, nina hakika katikati ya mwezi wa saba na tisa kiwanja kiwe kimekamilika, hapa hapa namuagiza Waziri wa Fedha alipe Bilioni 2.5 ili kiwanja hiki kikamilike.
Mamlaka ya Viwanja wa Ndege na Wizara husika ihakikishe malipo ya nyumba kando ya uwanja yafanyike haraka ili abiria watakaosafri na ndege zetu wapate sehemu nzuri ya kusubiri kabla na baada ya safari.
Nawapongeza pia serikali ya Mkoa wa Mara kwa Kazi nzuri na pia kwa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara kwa kuratibu na kusimamia kazi hii vizuri.”
Hapa hapa Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Mtambi alimuongoza Mgeni wake Katibu Mkuu wa CCM Taifa kuelekea Hospitali ya Rufaa ya Kwangwa na walipofika kisha hapa hapa Kanali Mtambi aliyasema haya,
“Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mara, ujenzi wa Hospitali umepitia awamu zote sita lakini awamu hii ndiyo umeshika kasi, Mama Samia amepambana mno na Mama Samia anatujali mno wananchi wa Mkoa wa Mara, siyo kwa sekta ya afya tu bali hata barabaraba, maji na sekta zingine huko kote, jamani huko pia zimemwanga pesa za kutosha na wewe Katibu Mkuu umekuja kuangalia utekelezaji wa ilani, kwa hakika kipekee kabisa nawaomba wana wa Mara, watambue kwa mema haya tuwe na shukrani kwa Mama Samia maana akufaaye kwa dhiki -ndiye rafiki wa kweli.”
Wakati shughuli hii ikiendelea Mwanakwetu alishuhudia ujio wa waziri Mdogo wa Siha Tanzania Dkt. Godwin Mollel nayeye kuwasalimu watu wa Musoma na kisha Katibu Mkuu CCM kuyasema maneno machache kwa wananchi wa Mkoa wa Mara.
Kikubwa Balozi Dkt Nchimbi akisema bayana kuwa Katibu Mkuu CCM hawezi kuwa na maneno mengi hapa hospitalini bali anawaacha wahudumu wa afya waendelee na kazi ili majukumu yao yafanyike na Watanzania wapone.
Baadatye Mwanakwetu alikutana na wanaccm wanne hapa Musoma Mjini na wao kutoa maoni yao juu ya ziara ya Balozi Dkt Nchimbi hapa Mara huku wakimpa heko tele.
Msomaji wangu kilichofuata baada ya hapo mambo yalimahamia Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Mara , huku nyimbo za CCM zikiipamba shughuli hiyo.
Mwanakwetu mtumishi umma alibeba begi lake na kurudi zake
ofisini, nayo CCM ikiendelea kumpamba Katibu Mkuu wao Balozi, Dkt .Emmanuel Nchimbi.
Mwanakwetu upo?
Haya yote ni ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa akiwa Wilaya ya Musoma hapa Mkoani Mara kumbuka ziara inaendelea haya ni ya siku ya pili tu.
Kumbuka
“Nitamualika Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Aje Kunywa Chai Ofisini Kwangu.”
Nakutakia siku njema.
0717649257




Post a Comment