Adeladius Makwega-Musoma MARA
Idara ya Elimu Mkoa wa Mara imesema kuwa mashindano ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa ngazi ya Mkoa huu yanaanza rasmi Alhamisi Aprili 10, 2025 ambapo wanamichezo hao wa ngazi ya Shule za Msingi na Sekondari wote watakuwa shule ya Sekondari Tarime kwa zamu .
Akizungumza mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Mara ndugu Geodfrey Kusaya, Afisa Elimu Mkoa huu Mwalimu Makwasa Bulega alisema,
“Kipenga cha kuanza michezo hiyo kimeshalia kwa Shule za Msingi Chini ya UMITASHUMTA wanaingia kambini.Kisha wakimaliza watatoa nafasi kwa Shule za Sekondari Chini ya UMISSETA na baada ya hapo zoezi hilo litahamia kw UMITASHUMTA na UMISSETA ngazi ya taifa.”
Mwalimu Bulega aliongeza kwa kuwa, hali ya maandalizi ipo vizuri ambapo Shule ya Sekondari Tarime ina uwezo huo na maandalizi yote yako vizuri, akizungumza haya mbele ya Kikao cha Wakuu wa Idara na Vitengo Mkoa wa Mara Afisa Elimu Mkoa wa Mara mwalimu Makwasa Bulega alinadi kuwa
“Mashindano ya UMISTASHUMTA kwa ngazi ya mkoa yakimalizika yanataa nafasi ya UMISSETA ngazi ya mkoa na tunafanya hivyo ili kuifanikisha michezo hiyo kikamilifu.”
Akizungunza katika viunga vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwalimu Bulenga alinadi kuwa UMISSETA ni umoja wa Michezo wa Shule za Sekondari Tanzania nayo UMITASHUMTA ni Umoja wa Michezo na Taalumu Kwa Shule Za Msingi Tanzania na michezo hiyo ilianza mwaka 1971 hadi ilipositishwa mwaka wa 2000 na kurejeshwa tena mwaka wa 2007 na baadaye ilipigwa dafrao na Ugonjwa KOVIDI 19.
“Baadaye ilirejea na sasa tunaendeleza libeneke la Michezo nchini Tanzania.
Wanafalsafa wa kale kama vile Plato na Aristotle waliona michezo na shughuli za kimwili kuwa muhimu kwa elimu, naomba ili likumbukwe siyo elimu ni muhimu kwa sababu ya michezo bali michezo ni muhimu kwa sababu ya elimu. Michezo iliyokamilika na ukuzi wa maadili, wakisisitiza jukumu lao katika kuunda tabia na kukuza ustawi wa kimwili na kiakili.
Hapa kuna mtazamo wa kina zaidi wa mitazamo ya baadhi ya wanafalsafa muhimu:
“Kwake Plato anasema Mazoezi ya kimwili yanayoaminika yalikuwa muhimu kwa ajili ya kukuza nidhamu binafsi na mtu aliyekamilika vizuri, hasa kwa wale wanaotaka kuwa viongozi au wanafalsafa, yeye alitetea ushiriki wa wanawake katika michezo, akiona kama njia ya kuimarisha maadili.”
Hata kabla ya kuwa mwanafunzi wa Socrates, Plato alikuwa mwanamieleka na alishiriki katika Michezo ya Isthmus, tukio muhimu la riadha katika Ugiriki ya kale. Jina halisi la Plato lilikuwa Aristocles, lakini alipata lakabu "Plato" maana yake "mpana"kwa sababu ya umbile lake thabiti michezoni akiwa mtu aliyekamilika.
Aristotle: Alisisitiza shughuli za kimwili kama wajibu wa kimaadili na njia ya kufikia maisha yenye usawa. Mawazo yake juu ya maadili mema, ambayo yanasisitiza ukuzaji wa tabia, yanafaa kuelewa jukumu la michezo katika elimu. Falsafa ya Kisasa ya Michezo: Falsafa ya mchezo kama uwanja wa kitaaluma ni mpya kiasi, lakini mtazamo wa kifalsafa wa mchezo wenyewe sivyo. Uchunguzi wa kifalsafa kuhusu mchezo huchunguza maswali kuhusu asili ya mchezo, dhima yake katika utamaduni wa binadamu, na vipimo vyake vya kimaadili. Falsafa ya michezo inachunguza historia ya michezo, mila zake, na nafasi yake katika jamii. Kitabu cha mwanafalsafa wa Yale Paul Weiss kiitwacho Sport: A Philosophical Inquiry" (1969) kinachukuliwa kuwa maandishi ya kwanza ya urefu wa kitabu katika falsafa ya michezo.
Naye Pierre de Coubertin, mwanzilishi wa Michezo ya Olimpiki ya kisasa, alikuwa na matokeo makubwa katika maendeleo ya elimu, michezo, na elimu ya kimwili. Utafiti wake wa kuleta mabadiliko nchini Ufaransa na hatimaye ulimwengu ulikuwa jambo ambalo wanaume wengi wangeshindwa kulitimiza.
Mwanakwetu alipokuwa anayatayarisha makala haya alimkumbuka ndugu yake Jemedari Said Bin Kazumari wakati huo tukisoma Ndanda Sekondari kati ya mwaka 1996-1998.Jemedari Said alikuwa Mwanamichezo bora shuleni akishiriki kila mara michezo ya UMISSETA Taifa katika timu ya soka ya Mkoa wa Mtwara na mara nyingi yeye ndiye alikuwa akiipa ushindi timu ya mkoa wa Mtwara na hata timu ya Ndanda Sekondari ilipocheza na MAABATE wa NDANDA. Kila aliporudi mashindanoni Jemedari Said alikuta tumeshafanya mitihani, alifundishwa vipindi vya ziada na kupewa mitihani na huku akifaulu vizuri .
Mechi ninayoikumbuka ilikuwa baina ya Kidato cha Sita (Akina Jemedari Mwanakwetu akiwa mshangiliaji ) na Kidato cha Tano akina Hamza. Jemedari Said alifunga mabao mawili na huku kidato cha tano cha Ndanda walipata bao moja kutoka Hamza.
Mwanakwetu kwa makala haya anawawatakia Idara Elimu Mkoa Mara usimamizi mwema na mzuri wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA kwa ngazo ya mkoa huu lakini wakumbuke mambo mawili;
Mosi,-Wanafalsafa wa kale kama vile Plato na Aristotle waliona michezo na shughuli za kimwili kuwa muhimu kwa elimu.Pili-Jemedari Said alikuwa Mwanamichezo bora shuleni akishirki kila mara michezo ya UMISSETA Taifa katika timu ya soka ya Mkoa wa Mtwara na mara nyingi yeye ndiye alikuwa akiipa ushindi timu ya mkoa wa Mtwara na hata timu ya Ndanda Sekondari ilipocheza na MAABATE wa NDANDA. Kila aliporudi mashindanoni Jemedari Said alikuta tumeshafanya mitihani, alifundishwa vipindi vya ziada na kupewa mitihani na huku akifaulu vizuri .
Watoto wetu wakitoka michezoni wafundishwe saa za ziada ndipo wapewe mitihani, maana maeneo mengi wakitoka michezoni wanapewa mitihani tu bila ya kupewa masomo ya ziada hili walimu wa michezo walisimamie .
Mwanakwetu Upo?
Kumbuka
“MICHEZO IFANIKISHE ELIMU-PLATO.”
Nakutakia siku njema.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment