Mwanakwetu aliamka asubuhi ya siku hii na akilini mwake akibebwa mzegamzega na taswira za Majaji wawili wa Mahakama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mhe. Jaji Jacobs Mwambegele na Mhe. Jaji Dkt. Paulo F. Kihwelo.Taswira hizi za jamaa hawa wawili kutoka mahakama ya Rufani ya Tanzania ilimjia Mwanakwetu tu kwa sababu moja kubwa maana katika dawati la Mwanakwetu, nyumbani kwake kuna Dawati la Ujamaa kulikuwa na nyaraka saba za sheria, ambazo zinawawahusu hawa majaji wawili yaani; Mhe. Mwambegele na Mhe. Dkt Kihwelo.
“A Compendium of Child Sexual Abuse Cases of Tanzania And Ireland-A short Version , 2025-Institute of Judicial Administration Lushoto(IJA),A Compendium Of Child Justice Cases- Institute of Judicial Administration Lushoto(IJA) na Exploring Judicial Culture In Tanzania- Institute of Judicial Administration Lushoto(IJA).”
Hivyo vyote vitabu vitatu vimeandikwa na Jaji Dkt. Paul F. Kihwelo akiwa kiongozi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto mkoani Tanga, hii ni Taswira nambali moja iliyombeba mzegamzega Mwanakwetu.
Taswira ya pili ilikuwa ni nyaraka nne za sheria na kanuni kutoka Tume Huru ya Uchaguzi;
“Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura za Mwaka 2024, Kanuni za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi za Mwaka 2024, Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Mwaka 2024 na Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024.”
Kwa hakika nyaraka zote saba Mwanakwetu alizipata mkoani Dodoma ambapo kulikuwa na shughuli ya Sheria, huku hizi nyaraka za Tume Huru ya Uchaguzi alipewa Bure lakini hivi vitabu vitatu vya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Mwanakwetu alinunua.
Mwanakwetu akiwa na taswira mbili za Bure na Nunua huku hii Taswira ya Nunua ikiwa ni ya Jaji Dkt Kihwelo na Bure ya Jaji Mwambegele. Taswira Nunua ilionesha namna hawa IJA chini ya Jaji Dkt. Kihwelo wanavyotunga vitabu na kuonesha kuwa taasisi yao ni ya taaluma wanatunga vitabu vya sheria ili jamii ijifunze, huku Mwanakwetu akitafuta nakala tepe(soft copy) ya vitabu hivyo lakini hakupata.
Kwa hakika tangu Mwanakwetu anunue vitabu hivyo vya IJA ameshavisoma kwa kina na huku hizi Kanuni na Sheria za Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tanzania nazo amezisoma vizuri neno kwa neno.
Mwanakwetu akiwa katika tafakari yake juu ya Jaji Dkt. Kihwelo, taswira NUNUA na Chuo cha Uongozi wa Mahakama wao wanatoa elimu ya sheria tu kwa vijana wanaokwenda hapo na wakitoa mafunzo kazini hadi kwa MAJAJI naye Jaji Mwambegele yeye na BURE ya Tume Huru ya Uchaguzi wanatoa hudumu kubwa ambayo kwa hakika inatoa muelekeo wa taifa letu la Tanzania kila unapofanyika uchaguzi kwa ngazi ya Diwani, Mbunge na Rais.
Hapo hapo Mwanakwetu akamuweka kando Jaji Dkt. Dkt Paul F. Kihwelo na Chuo cha Uongozi wa Mahakama na kumsogeza karibu Mhe. Jaji Mwambegele na Tume yake huru ya Uchaguzi nchini Tanzania, Mwanakwetu akajiuliza je mwenendo wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Tanzania unaridhisha?
Nini maoni ya baadhi ya Watanzania waliyokutana na Mwanakwetu katika hili?
Mwanakwetu alimkumbuka jamaa mmoja ambaye alikutana naye;
“Kaka Makwega, sisi mambo mengi tunayafahamu hasa wakati wa chaguzi, unajua wakati wa Uchaguzi wa Serikalia za Mtaa kuna pahala kulitokea vurugu, watu wakaenda, pale awali hakukuwa na ugomvi, wananchi wamepiga kura vizuri, kwa amani shida ikawa wakati wa kutangaza matokeo. Jamaa walipoenda ndiyo matokeo yakatangazwa na vuruga kuanza tangu kwa mgombea mmoja na wasimamizi wa uchaguzi, hilo likaleta maneno na vurugu
Vijana wa Polisi walifanya kazi yao ngumu na kwa tabu katika eneo ambalo hakukuwa na ugomvi awali chama kimoja kilishatazama kibra kikiona kilivyoshindwa.
Gari walilopanda likapata nyufa ya kioo kutokana na kurushiwa mawe na wanakijiji. Huku waliosaidia kutangaza matokeo wakakimbia kurudi walipotoka na Mungu bahati kioo hakivunjika lakini kama kioo kingevunjika wangeumia.”
Ndugu huyu anasimulia kuwa kama angetangazwa aliyeshinda kwa haki wananchi wasingefanya vurugu, wala gari lisingerushiwa mawe, kioo kisingepata nyufa na wala risasi hewani zisingelirushwa na kule ni kuhatarisha amani ya eneo husika kusingali kuwepo kabisa.
Gari lililopata hitilafu baadaye iliulizwa kisa nini na maelezo yaliyopotolewa ilioneka kuwa Hilo Siyo Tatizo, lakini jamaa waliyokuwepo siku ya tukio wanasema je kama wananchi wale wangeweza kuvunja kioo na kuwadhuru ingekuwaje?
Kama mmoja wapo angeumia vibaya au kufariki je ingekuwa? Au Jibu Ingekuwa Hilo Siyo Tatizo?
Mwanakwetu anasikiliza hoja hizo moja baada ya nyingine, kisha jamaa huyu akasema :
“Malalamiko ya Watanzania dhidi ya Tume huru ya Uchaguzi ni sahihi,. Inawezekana Jaji Mwambegele hana shida, moyo wake ni mwema lakini shida yake Jaji Jacob Mwambegele anafanya kazi na watu ambao hawafahamu tabia zao, yeye amekaa mahakamani na kuhukumu kesi huku wanasheria wa pande mbili wakimpa taarifa kisha yeye anaitoa hukumu.
Kama mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Jaji Mwambegele alitakiwa awe huru wa kuchagua watu wa kufanya nao kazi tangu Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa, wasimamizi wa Uchaguzi ngazi za Mikoa, Wilaya Majimbo hadi vituo vya kupiga kura na Jaji Mwambegele asiingiliwe na taasisi yoyote ile kuifanya kazi hiyo, huku akisaidiwa na taasisi za dini kulifanikisha zoezi hilo. Vinginevyo Tume Huru haiwezi kufanya kazi na watu wale wale, wenye tabia zile zile. Wanaoamini kuwa Hilo Siyo Tatizo.
Hali hii inaharibu sana hata heshima ya majaji kutoka Mahakamani za Tanzania kuwa wanasimamia uchaguzi kila baada ya miaka mitano lakini nyakati za uchaguzi kura feki zinazagaa mitaani, mabegi kwa mabegi.
Hili linajenga dhana mbaya kuwa pengine hata Majaji wanaopewa jukumu katika Tume ya Uchaguzi na wao wanashirikiana na uhalifu huu.”
Ndugu huyu akasema kama kweli Jaji Mwambegele ana nia njema moyoni mwake na Mungu wake na kulinda jina lake na heshima ya Mahakama ya Rufaa, yako mambo mengi alitakiwa kuyafanya kazi mapema lakini hajafanya hata moja. Mojawapo ni kuwatilia shaka baadhi ya watendaji wa Tume Huru ya uchaguzi, anachoweza kufanya sasa anatakiwa kujiuzulu na kutoka nje ya mchezo, maana ameshachelewa maana uhakika na watu anaofanya nao kazi kuwa wana nia nia njema ni ngumu , yeye alikuwa mahakamani watu wanawafahamu baadhi ya watu kwa tabia zao, nyakati za uchaguzi zikifika, kwa hiyo kujiuzulu itakuwa salama kwake.
Nakuomba msomaji wangu hifadhi haya makala.
Mwanakwetu Upo?
Kwa hakika hii ni tafakari ya Mwanakwetu juu ya Tume Huru ya Uchaguzi ambayo imembeba Mwanakwetu tangu nyaraka zile saba za Sheria nyumbani kwake, zikasafiri na wewe msomaji wake tangu kwa Mhe. Jaji Dkt Paul F. Kihwelo na hadi kwa ndugu yetu Mhe. Jaji Jacobs Mwambegele.
Jaji Mwambegele wewe ni ndugu yetu, leo Mwanakwetu natumia neno NDUGU . Mhe. Jaji nakuomba uyasome makala haya mara tatu, kisha uitazame na dhamiri yako, mbele ya Mungu, huko wako watu wanaosema HILO SIYO TATIZO. Hawa wanaosema haya ni watu hatari mno,
Kwa hakika kila baada ya miaka mitano Watanzania tunafanya Uchaguzi Mkuu na hii ni haki yetu na hakuna mwaka hata mmoja katika historia ya Tanzania uchaguzi ulikosekana, huku chaguzi zikifanyika lakini sauti za wizi wa kura zimeinuka na kulia mno.
Swali la Mwanakwetu linalobaki Je NDUGU Mwambegele huku kwao alikozalia ni bingwa kufanya miujiza? Na ataweza kuzuia hali hii, Je ataweza kuja na mwalubaini huo?
Kwa ukweli wa Mungu Mwanakwetu hana hana hana hakika na hilo.
Mwanakwetu upo?
Je makala haya niyahitaje?
Taswira Mbili za Majaji Wawili, Hilo Siyo Tatizo au Jaji Mwambegele Anawajibu Ajiuzulu NDUGU Mwambengele Hawezi kufanya Miujiza .
Mwanakwetu anachagua NDUGU Mwambegele Hawezi Kufanya Miujiza .
Nakutakia Siku Njema.
0717649257




Post a Comment