Adeladius Makwega-Musoma MARA
Mkuu wa Wilaya ya Musoma mhe. Jumaa Chikoka Aprili 10, 2025 amewataka WasaniI wa Filamu Wilayani Musoma mkoani Mara kukumbuka kuhamasisha Watanzania kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025, huku akisema serikali inatambua mchango wa kazi sanaa katika kukuza umoja wa kitaifa.
Haya yamesemwa na Afisa Tarafa wa Musoma Mjini ndugu Ahmad Kanuni alipokuwa akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Musoma katika hafla ya udurusi wa filamu inayofahamika ACHA NIKUPENDE yenye saa 2 na dakika 17, yenye kubeba maudhui ya umuhimu wa dini kuachana na imani za ushirikina.
“Kwa sasa tunaona tasnia ya filamu Wilaya ya Musoma inakua kwa kasi, kikubwa ninachowaambia mjitahidi kuwa na kazi bora zitakazo weza kushindanishwa na kazi za mikoa mingine na hata nje ya Tanzania sokoni la Musoma linaweza kuwa Nairobo na hata Kampala kazi zetu ziwe bora.”
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa Kampuni ya IDM Arts ndugu Michael Majura amesema kuwa hadi sasa wameimaliza, kazi hii kukamilika ni gharama nyingi, anawashukuru wadau wote waliowashika mkono, kazi iliyo usoni mwao kwa sasa ni kutafuta soko na wakiimiza kikao hicho watafanya maboresho ya mwisho huku akiomba wa Watu wa Musoma na Tanzania nzima kuwaunga mkono kununua kazi hiii.
Mwishoni kazi hii ya ACHA NIKUPENDE ilingizwa katika maombi nia mwalimu wa dini kutoka Kanisa la AIC NYASHO Elisha Malanja
0717649257
Post a Comment