USINGIZI WA MANG’AMUNG’AMU

 

Adeladius Makwega-MBAGALA

Mwanakwetu kauchapa usingizi mzito katika kitanda chake cha banko cha urithi wa bibiye Hedwiki Omari Binti Mkomangi hapa Mbagala , kitanda cha telemka tukaze, gafla akasikia simu yake inaita kwa muda mrefu kidogo, kwa kuwa alikuwa amechoka hakuipokea, akaendelea kuupiga usingizi huo matata, simu ikaendelea kuita , sasa ikawa kero, akaamua kuipokea..

“Asalaam aleikuum Mwanakwetu! Kaka nimeulizia bei ya moja ni shilingi 16,500/- mimi ninahitaji manne.”

Mwanakwetu akamjibu huyu jamaa huku akiwa na lepe za usingizi mzito akisema saaawa nitakutumia .

Jamaa huyu akaendelea kuongea,

“Umemuona Tundu Lissu amekwenda Zanzibar na kapiga mbonge dalizi, jamaa asije akawa anakwenda Kijitoupele kwa rafiki yako kumshawishi awe mgombea mwenza wa 2025, kama vile 2015 kwa Juma Duni Haji maana nyie si mmeshamaliza mambo, sisi ndiyo tunaanza.”

Hapo hapo usingizi wa Mwanakwetu ukakata, akamuuliza huyu jamaa unasemaje? Jamaa akarudi sentensi hii,

“Umemuona Tundu Lissu amekwenda Zanzibar na kapiga mbonge dalizi (kanzu), jamaa asije akawa anakwenda Kijito upele kwa rafiki yako Shamsi Vua Nahodha kumshawishi awe mgombea mwenza wa 2025 kama 2015 kwa Juma Duni Haji.”

Mwanakwetu akacheka sana kisha akaomba picha hizo na akapewa hapo hapo akilini mwa Mwanakwetu yakamjia haya,

“Inawezekana yakawa ya kweli, maana Kila siku Shamsi Vua Nahodha, tangu Asubuhi, Mchana na sasa Jioni, tangu mvua na sasa Jua Limezama yeye anasubiri, atasubiri mpaka kiama? Nyie mbona hamna subira?”

Jamaa akasema nakwambia Mwanakwetu Unafikiri 2025 ni Kumsukuma Mlevi?


 

Hapo Mwanakwetu aliyekuwa na mang’amung’amu na lepe la usingizi awali yamekata kabisa na simu bado ipo hewani jamaa akauliza akauliza Mwanakwetu tupo sambamba akajibiwa ndiyo.

Mwanakwetu na hili la mwisho;

Umemuona Mama yake Ummy? Nikauliuza Ummy yupi ? Jamaa akajibu Ummy Mwalimu , wapi ? Jamaa akaijibu mtandaoni, jamaa akatuma picha kama ilivyo.

Mwanakwetu alipoiona picha hii akacheka sana kisha akasema,

“Kumbe mama yake Ummy Mwalimu yupo vizuri sana, wamo sana, anaweza huyu kuwa hata First Lady, maana tangu 2021 Tanzania imemmisi FIRST LADY.”

Jamaa akasema Mwanakwetu mama yake Ummy awe FIRST LADY? Mwanakwetu akajibu naam. Jamaa akasema sasa vita na wazee wa kidigo inawezekana?

Mwanakwetu akajibu hilo dogo,

“Wazee wa Kidigo hawawezi vita kabisa , lazima wawe wapole, mama huyu anatakiwa awe First Lady safari ni za Magogoni na Chamwino. Wadigo/Wabondei / Wasambaa wote kiboko yao alikuwa Dossa Azizi Ally, Yule alikuwa mzee wetu kwa hiyo hawana shida.”

Jamaa akacheka sana , akiuliza unamjua Dossa Aziz? Akajibiwa sana tu Tangu Mtoni Mtongani hadi Mtoni Azizi Ally. 


 

Mjadala huo ulikuwa wa vicheko tele ukijengwa na mambo mawili, kwanzai juu ya Safari ya Lisu Zanzibar na Urembo wa mama yake mh Ummy Mwalimu.

Simu hiyo ilipokata ndipo Mwanakwetu akaamua kuyatayarisha makala haya.

Mwanakwetu anasema nini slu ya leo?

Kwa hakika simu hii ya mapema mapema imenipa tafakari tele mie mwana wa Makwega hasa juu ya Urembo wa mama yake Ummy Mwalimu na husuda ya Mwanakwetu kuwa mama huyu awe Fist Lady. Mwanakwetu anawaomba Wadigo, Wabondei na Wasambaa wawe wapole.

Jambo la pili ni hii Safariaya Tundu Lissu huko Zanzibar, ikiibua maswali kwa wadauwa  wa siasa za Tanzania huku wakidhani kuwa inawezekana Tundu Lissu yupo katika harakati za kumsaka mgombea mwenza, wengine wakidokeza kuwa itapendeza kama akiwa Mzee Kijitoupele , ndugu yetu Shamsii Vuai Nahodha maana amesubiri sana na sasa subiri hiyo inatosha.

Jmabo mwisho picha hizi mbili zinatoa tafakari kubwa ya Watanzania wanafikiria mambo mengi sana ambayo Mwanakwetu hana hakika kama wanasiasa wa Tanzania wanayawaza haya yote.


 


 

 

Mwanakwetu upo?

Je makala haya niyaitaje?

Unafikiri mwaka wa 2025 Kumsukuma Mlevi.? Mama Huyu Anafaa Kuwa First Lady au Usingizi wa Mang’amu ng’amu?

Mwanakwetu anachagua ;

“Usingizi wa Mang’amung’amu.”

Nakutakia siku Njema.

makwadeladius@gmail.com

0717649257

 



 

 

 

 

 

0/Post a Comment/Comments