Adeladius Makwega-MBAGALA
Katika matini ya I na II nilikusimulia juu ya Katibu wa Waisilamu wa “MASJID RAHMAN BUTIAMA.” wakati wa ujenzi wake mwaka 1998 Sheikh Azizi Magambo Bini Rubare (pichani) ambaye nilipokuwa nazungumza naye alinidokeza mambo kadhaa, naomba msomaji wa matini hii kwa leo niyatilie maanani mambo makubwa mawili tu.
Kwa hisani yako nianze na jambo la kwanza, kiasi cha pesa kilichosalia baada ya msikiti na majengo yanayozunguka msikiti huo kukamilika kilikuwa ni Tsh 23/- milioni.
“Kwa hakika tulibakiwa na Tsh 25 milioni kiasi chaTsh milioni mbili na ushehe zilitumika kugharamia asilimia kwa malipo kwa wale waliokuwa wakifanya kazi hiyo ya ujenzi na ndiyo maana ikabaki milioni 23 tu.”
Binafsi nilisema moyoni kuwa kama ujenzi wa msikiti huo uliweza kubakiza kiasi hicho kwa mwaka 1998-2000 maana yake kamati zote za ujenzi zilitimiza wajibu wao ipasavyo.
Huku watumishi wa umma wa wakati huo kama vile ndugu yetu Rafael Mkanzabi ambaye awali alikuwa msaidizi wa Mwalimu Nyerere alitimiza wajibu wake vizuri sana.
Ndiyo kusema maombi ya Waisilamu wa Butiama kumuomba mwajiri wa Rafael Mkanzabi wakati huo kumbakiza ndungu huyo halikuwa kosa bali walitambua umuhimu wake na uwezo wake wa kiutendaji tangu akiwa na Mwalimu na hata Mwalimu Nyerere alipofariki dunia.
Waisilamu wa Kijiji cha Butiama wanamkumbuka sana Rafael Mkanzabi si kwa sababu alikuwa Msaidizi mwalimu tu, mwalimu alikuwa na wasaidizi wengi Mkaziba hakumbukwa kwa kuwa alifanya kazi na mwalimu la hasha bali kwa kuwa yeye ndiye aliwatia moyo na kuwambia kuwa hata kama mwalimu amefariki pesa zenu zipo pahala salama na ujenzi wa msikiti lazima ukamilike na ufanyaji wake kazi wa kiuadilifu.
Naomba msomaji wangu ufahamu kuwa hata watu wa kawaida kabisa wanamtambua mtu mwema kwa vipimo vyao pia wanamtambua mtu mwovu kwa vipimo vyao.
Msomaji wangu swali kwako je wewe ni mtu mwema au mtu mwovu?
Pengine jina hili la Rafael Mkazabi leo hii lisingalikumbukwa na mtu yoyote kama ndugu yetu huyu angelifanya tofauti. Kwa hakika vyovyote iwavyo, leo hii nina hakika kati ya ndugu wa damu wa Rafel Mkanzabi inaweezekana anayasoma matini hii ndugu yenu aliwawakilsiha vizuri anuani ya jina lenu ilitumiwa vizuri.
Waisilamu wa Butiama nilipowauliza ndugu Rafael Mkanzabi alipotoka Butiama alikwenda wapi? Walinijibu kuwa alihamshiwa Iringa akiwa Afisa Usalama wa mkoa huo, kwa wakati huo.
Nafahamu wasomaji wa matini hizi wana desturi niliyoijenga ya kunipa majibu ya baadhi ya maswali. naweka mezani swali juu ya alipo ndugu yetu Rafael Mkanzabi leo hii, naomba majibu msomaji wangu.
“Swali la kujiuliza ni kwa nini Mwalimu Julius Nyerere akiwa hai, huku akifahamu kuwa pesa za ujenzi wa msikiti huo zingetosha kuukamilisha tangu msingi hadi kumalizika, ilikuwaje Mwalimu Julius Nyerere alitoa masharti mawili kati ya matatu aliyosema?
Yaani Waisilamu wa Butiama kupeleka mawe tripu 120 na kupeleka mchanga tripu 120 katika eneo la ujenzi?
Hoja ya pili ya matini hii ipo katika kulijibu swali hilo ambalo binafsi nilimuuliza Sheikh Rubare.”
Kwanza Sheikh Rubare aliungama wazi kuwa Waisilamu wa Butiama walifanya kazi hiyo vizuri mno, wakishirikiana na kila mmoja wao. Kushindwa kukamilisha hilo kilikuwa kitendo cha aibu kwao na kitendo cha kuiabisha dini yao UISILAMU, ambapo kufanya hivyo ilikuwa ni jambo ambalo haliwezekani kabisa.
Mapambano ya kuifaya kazi hiyo yalifanyika usiku na mchana. Dhana ya mwalimu Nyerere kuagiza hilo inatokana na Mwalimu Nyerere kutambua kuwa msikiti huu utakapokamilika utakuwa mali ya Waisilamu wa Kijiji cha Butiama.
Pia Mwalimu Nyerere alifanya hivyo ilikujenga dhana ya umiliki wa msikiti huo kwa Waisilamu wenyewe wa Kijiji cha Butiama.
Mwanakwetu anaiweka kalamu yangu chini kwa kukukumbusha kuwa Apri13, 2022 tunakumbuka miaka 100 tangu Mwalimu Nyerere kuzaliwa, tambua kuwa mandhari ya msikiti huu unavyoiona leo hii Mwalimu Nyerere hakuiona kwa macho yake kwani alifariki mapema wakati kazi hii ndiyo ilikuwa inaanza.
Mwanakwetu upo?
“MISINGI THABITI NA TIMILIFU.’
Raha ya Milele uumpe Eee Bwana na Mwanga wa Milele Umuangizie apumzike kwa amani Amaini.
makwadeladius@gmail.com
0717649257
Post a Comment