Adeladius Makwega-SINGIDA/SHINYANGA
Mwanakwetu anasafiri akielekea mazikoni, akiwa anatafuta usafiri aliambiwa kuwa njia za kupitia ni mbili tu;
“Musoma Serengeti Arusha nauli shlingi 40,000/= au Musoma Singida Manyara Arusha nauli 60,000/=, basi ya kupitia mbungani linatokea Tarime na linaondoa alfajiri na basi linalopitia Singida Manyara linaondoa saa 9.30 alasiri.”
Mkataji wa tiketi alishamkatia Mwanakwetu basi la kupitia mbugani, hapo hapo mkataji akaulizwa dazani ya maswali; Je basi lako lina chaji akajibu ipo kwa dereva tu , akaulizwa swali lingine mbungani dunda dunda bado zipo? Jamaa akajibu baba bado zipo. Hapo hapo akagairi na kukata basi ya kutipitia Singida Manyara kisha Arusha.
Kiti cha kwanza kilichokuwa wazi kilikuwa namba 14, nikachukua hicho hicho na kukaa zangu na kuanza safari hiyo kuelekea Arusha. Basi hili kwa kuwa lilianza safari Musoma Mjini kwa hakika lilikuwa tupu lakini watu walikuwa wanapandia njiani. Kwenye mtandao awali niliona hata kiti namba 13 kilikuwa na abiria.Tulipofika Bunda wakapanda abiria kadhaa, hapo nikiwa na lepe na usingizi lenye wingi na mang’amung’amu.
Shikamoo baba, naomba nipite kiti changu namba 13. Nikajibu marahaba na kisha kumpisha binti huyu ambaye alikuwa na mtoto mdogo. Mama huyu akakaa na kuendelea na safari hiyo.
Mwanakwetu tangu akiwa Bweri/ Nyabange Musoma mkoni Mara alichukua simu yake na alikuwa anayasikiliza makala ya Magazeti ya Ujerumani ya Agosti 28, 2013 na makala hiyo yalitayarishwa na Abdul Mtulya, haya ni makala ya miaka mingi.
“Mgogoro wa Syria umekuja katika wakati mbaya ambao wanasiasa wa Ujerumani wako katika pirika pirika za uchaguzi unaowagusa wanasiasa wa upande wa shoto, ukiwaangalia wanasiasa wa upande wa serikali na wanasiasa wa upande wa upinzani wote kwa utatu wao wanajaribu kujiepuka suala la mgogoro wa Syria katika kampeni zao, Wanasiasa hawa wanatambua kuwa suala la vita halitawapatia kura, ikiwa wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanadai kuwa majeshi ya serikali ya Syria walitumia gesi ya sumu ,
Wanasiasa wa Ujerumani hawataweza tena kupiga chenga suala la Syria, Wahariri hao wanakumbusha suala la maadili ya jamii ya Ujerumani kuwa Katiba ya taifa lao iliyojengwa katika msingi wa haki za binadamu inawawajibisha Wajerumani kuwa macho dhidi ya udhalimu na yoyote anayefumbia macho udhalimu mbele ya picha zinazoonesha raia waliouliwa na gesi ya sumu anapwaswa afunge domo lake hata hivyo inapaswa kujihadhari na ushetani wa kulipiza kisasi…”
Safari hii inaendelea, huyu binti mrembo wa Kichaga akapigiwa simu nadhani ya mumewe, akiuliza umeshapanda basi?Akajibu ndiyo, ila wale madalali walichukia sana nilivyowaonesha tiketi yangu ya kukata online, wakisema sista unatunyima miambimiambili uwe unakuja kukata hapa dada yetu. Safari ikiendelea.
Binti huyu huku akimbeba mtoto wake vizuri, akauliza baba wewe umepandia wapi? Nikamjibu nilipandia Musoma mama, kisha akauliza tutafika Arusha saa ngapi? Nikamjibu mimi sifahamu njia hii, sijapita hata mara moja kwa safari za jioni. Mama huyu akaendelea kuuuliza kwani baba wewe unakwenda wapi?
Majibu yalikuwa haya
“Mama mimi nakwenda Lushoto Tanga, huko kuna msiba kuna mama yangu mmoja anaitwa Elifred Sebastian Kolowa , ambaye alikuwa mke wa Askofu wa kwanza kwanza Wazalendo wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt Sebastian Kolowa, amefariki dunia,mumewe alifariki tangu mwaka 1992, ninakwenda mazikoni.
Askofu Dkt . Sebastian Kolowa alikuwa MKUU wa KKKT tangu mwaka 1976-1992 na pia alikuwa Askofu wa mwanzo mwanzo Mzalendo wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki DKMs KKKT.”
Mama huyu akasema jina hilo analifahamu vizuri, hata yeye anakwenda Moshi kumzika kaka yake mkubwa, tumbo moja akiongeza kuwa asipokwenda ndugu zake hawawezi kumuelewa kwa madai ya umbali na gharama, Mwanakwetu akampa pole ya msiba huo, binti huyu kumpa pole ya Mwanakwetu ya msiba ya Bibi Kolowa.
“Baba nimelipa 62, 000/= ni pesa nyingi , Baba Watanzania tunalia kwa mengi, nakwambia baba yangu, kama Magufuli angekuwa hai hii njia ya Musoma kupitia Mbungani Serengeti Arusha ingekwisha tengenezwa na hadi sasa na tungekuwa tunapita .”
Gafla simu ya Mwanakwetu ikajichezesha yenyewe wimbo huu,
1
Jina la Yesu, salamu!
Lisujudieni, Lisujudieni;
Ninyi mbinguni, hukumu,
Na enzi, enzi, enzi, enzi,
Enzi enzi, enzi na enzi mpeni.
2
Enzi na apewa kwenu,
Wateteea dini, Watetea dini;
Mkuzeni Bwana wenu
Na enzi, enzi, enzi, enzi,
Enzi enzi, enzi na enzi mpeni.
3
Enyi mbegu ya rehema,
Nanyi msifuni, Nanyi msifuni;
Mmeponywa kwa neema,
Na enzi, enzi, enzi, enzi,
Enzi enzi, enzi na enzi mpeni.
4
Wenye dhambi kumbukeni,
Ya msalabani, Ya msalabani,
Kwa furaha msifuni,
Na enzi, enzi, enzi, enzi,
Enzi enzi, enzi na enzi mpeni.
5
Kila mtu duniani
Msujudieni, Msujudieni;
Kote-kote msifuni,
Na enzi, enzi, enzi, enzi,
Enzi enzi, enzi na enzi mpeni.
6
Sisi na wao pamoja tu
Humo sifani, Humo sifani;
Milele sifa ni moja,
Na enzi, enzi, enzi, enzi,
Enzi enzi, enzi na enzi mpeni.
Safari inaendelea , sasa Mwanakwetu akawa na ujirani na maneno na huyu binti, huyu binti akalala usingizi na mtoto wake, kiwiliwli kipo katika mapaja ya huyu binti na kichwa cha mtoto kipo katika mapaja ya Mwanakwetu, mapaja ya Mwanakwetu hayajazoeza kumbeba mtoto muda mrefu, Mwanakwetu kapewa kazi na mtoto huyu alikuwa na afya njema, hilo likampa tafakari nzito Mwanakwetu juu ya akina mama wanavyoteseka na watoto wao safarini.
Mwanakwetu macho wazi akawa anatafakarii madhara ya barabara ya kuzunguka inatumia pesa nyingi , gharama kubwa ya mafuta na muda safarini akasema kwani lami ikipita mbungani ya Serengeti shida nini? Majibu aliyopata yalikuwa haya.
“Barabara ya lami katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti haikujengwa kutokana na matatizo ya mazingira na uamuzi wa mahakama. Wasiwasi wa kimazingira Barabara hiyo ingekatiza katika eneo la mbali la kaskazini mwa hifadhi. Ingevuruga uhamiaji mkubwa wa Serengeti. Ingedhuru idadi ya nyumbu na wanyama wengine kama pundamilia. Ingeathiri wanyama wanaowinda wanyama wengine kama simba na duma. Ingeongeza trafiki kupitia mfumo wa ikolojia. Uamuzi wa mahakama Mahakama ya Afrika Mashariki (EACJ) ilitoa uamuzi dhidi ya mpango huo mwaka wa 2014.
Mahakama hiyo iliamua kuwa barabara hiyo itakiuka mkataba wa kikanda unaohimiza matumizi endelevu ya rasilimali. Mahakama ilikubaliana na hoja ya mlalamikaji kwamba barabara kuu itakuwa na athari mbaya zisizoweza kutenduliwa”
Maelezo haya kwa Mwanakwetu hayakutosha akapata maelezo mengine ambayo yalikuwa haya.Serikali ya Tanzania inaomba idhini ya Unesco kuboresha barabara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti Kaskazini baada ya mpango wake wa awali wa kujenga barabara ya lami katika hifadhi hiyo kugonga mwamba. Serikali ilikuwa imepanga, kati ya mwaka 2005 na 2012, kujenga barabara kuu ya lami yenye urefu wa kilomita 452 kuunganisha Arusha kaskazini mwa Tanzania hadi Musoma kwenye mwambao wa Ziwa Victoria lakini ikasusia mpango huo baada ya kufunguliwa kesi ya madai na vikundi vya ustawi wa wanyama vinavyopinga barabara hiyo kupita Serengeti.
Maelezo haya yaliendelea kunadi kuwa,“Machi 10 , 2024 aliyekuwa msemaji wa Serikali ya Tanzania Mobhare Matinyi alisema kuwa Serikali yao imaandaa nyaraka moja na kuiwasilisha UNESCO shabaha ni kuomba hilo. Machi 2011, Serikali ya Ujerumani ilitoa ufadhili wa kujenga barabara mbadala kupitia eneo la kusini mwa hifadhi hiyo hadi Musoma, lakini mpango huo ulisitishwa na serikali ya Tanzania. Serengeti inajulikana kwa uhamiaji wake wa kila mwaka wa nyumbu, ambapo nyumbu milioni 1.5 na wanyama wengine huvuka Mto Mara hadi Hifadhi ya Kitaifa ya Masai Mara nchini Kenya, jambo ambalo huvutia umati wa watalii kutazama mataifa haya kujipatia fedha za kigeni.
Binti huyu akaamka katika ndoto akisema,“Yaani baba chupuchupu gari letu ligongane, si umesikia watu wamepiga kelele Baba we acha tu, misiba inapotokea inatuletea hasara, kama unavyoona mimi nakwenda kuzika Moshi kwa gharama tele, hayo ni maamuzi ya Mungu, hata msiba wa Magufuli ni hasa kubwa kwa Tanzania, maono yake , alivyo kuwa na msimamo alivyokuwa anajiamini namna walivyokuwa wanamuamini, haya mambo hayaji bure ule ni mtaji uliyopotea ardhini
Nilipofuatilia mawasiliano yake ya simu, huyu binti wa Kichaga nilibaini alikuwa kama mtumsihi wa serikali mwenye watoto kama watatu. Safari inaendelea tukatifa kituo cha basi kizuri hivi, binti huyu akasema baba una mia tano ya karibu ninue kitu? Nikatoa shlingi 500/= ya sarafu nakumpa akanunua nadhani pipi na kumkaribisha Mwanakwetu, nikamjibu asante.
Binti huyu akasinzia tena naye Mwanakwetu akawa anasikiliza makala za Abdul Mtulya na hii ni ya Agosti 28, 2013.Mhariri wa gazeti hili anasema kuwa Christian Wulff Rais wa Ujerumani anayeshitakiwa hakufaa kuwa Rais wa taifa hilo, yeye alikuwa rais wa ngekewa, hivyo ilikuwa sahihi kwake kujiuzulu Urais huo wa Ujerumani. Wahariri hao wanaongeza kuwa Wulff kama binadamu labda tabia yake ilikwenda kombo lakini mabaya yanayazungumziwa dhidi yake na waliokuwa karibu naye yanakwenda mbali mno, yanatiwa chumvi, haya yanayozungumzwa yanapaswa kuwa mfano kwetu sote.
Kumbuka msomaji wangu Mwanakwetu anasafiri kutoka Musoma kwenda Arusha/Moshi, Binti huyu wa Kichaga akaamka yeye na mwanawe akawa analalamika baridi kali baridi kali ,akiomba nimuitie kondakta lakini alikuwa mbali kidogo, kondakta kijana akaja na kusema mama ahamia kiti kingine. Mama/binti huyu akagoma kutoka hapa alipo Mwanakwetu, tukaenda mwendo mrefu baridi ikawa kali mtoto wake akaanguka kilio, huku akimbembeleza, naye Mwanakwetu akisaidia kulea, Mungu bahati mtoto huyu alipewa nyonyo ya mama na kutulia tuli nyoyo ya mama ni tamu sana.
Baadaye mtoto akakomelewa na chakula kutoka katika chupa na kula vizuri. Chakula hiki kilikuwa kinanukia vizuri sana, Mwanakwetu akastajabu kumbe Wachaga wa siku hizo hatari kwa mapishi yao! Baadaye hali ilikuwa ya utulivu sana binti na mtoto wake wakapitiwa na usingizi mzito tena
.
Mwanakwetu yu macho mara akamkumbuka Bibi Kolowa enzi za uhai wake, naye Mwanakwetu akiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lushoto. alimpigia simu na kumsalimia kisha kumuita nyumbani kwake, akatoka alipo vizuri, kisha kufika nyumbani kwake anakampatia chai nzuri na kusaini kitabu cha wageni na kufanya naye mazungumzo marefu akisema.
“Baba unapokuwa kiongozi kwa ngazi yoyote. wewe ni Mchungaji wa Kondoo, kondoo wapo aina tatu wale wanaoitika haraka ukiita, wapo ambao hawaitiki ukuita na wapo ambao wanaitika baada ya muda wewe kuita, baba hao wote ni kondoo wako, lazima uwachunge kila siku inayokwenda kwa Mungu.
Mungu alivyomwema yule anayeitika haraka anaweza asitoe maziwa, yule anachelewa kuitika akawa na uzazi bora, huyu anayeitwa na kuchelewa kuitika akawa akizaa watoto wake anawatunza vizuri na wote anawakuza salama,.
Baba wote ni Kondoo wako, ukisema huyu ananisumbua machungani nimchinje hapo utashindwa uchungaji maana mwneye kondoo pengine wewe upo kibaruani tu.”
Siku hiyo Mwanakwetu alipozungumza na Bi Kilowa kisha kurudi nyumbani kwake ujumbe hua aliupata na kuuelewa sijuhi wewe unayeyasoma makala haya.Haya Mwanakwetu anayakumbuka tu lakini yu safarini.
Safari inaendelea na walipovuka Shinyaga binti huyu safarini alianza kutapika kwa muda mrefu Shinyanga Tabora yote, binti anatapika, Mwanakwetu kabeba mtoto watu wanashangaa hakuna aliyeamka kuja kutoa msaada hata mmoja. Nikasema moyoni ili Mwanamke aweze kusafiri kwa amani kutoka hatua moja kwenda nyingine kuna wajibu akina mama kuwa jirani na waume zao ili mambo yaende vizuri na hili hata kwa wanaume na wake zao pia.
Katika basi hili la watu 60 hakuna mwingine eliyewiwa kumsaidia mama huyu zaidi ya Mwanakwetu na huyo kondakta, watu hawataki kushika matapishi ya watu, Jamani Tubebeane Matapishi, tulipofika Hoteli ya Singida mama huyu akamuomba Mwanakwetu baba wa Hiari abakie na mtoto na yeye aende akaweke mambo sawa mariwatoni, kweli alifanya hivyo kisha Mwanakwetu kwenda na yeye kuweka mambo sawa.
“Naomba niwaambie wanasheria, mahakimu na majaji katika hali ya ugonjwa hakuna shambulio la aibu, watu wanaangalia namna ua kuokoa uzima wa binadamu siyo kila kitu ni sheria, sheria inafanya kazi katika baadhi ya mazingira.”
Binti huyu akanunua chakula lakini Mwanakwetu hakufanya hivyo, binti akauliza kwanini? Nikamjibu dada hata hamu ya kula sina. Basi likapiga gia kuendeleaa na safari ya Arusha/ Moshi. Safari ilienda vizuri hadi saa 11. 45 ya asubuhi likafika Arusha Mjini na kuwekwa mafuta, binafsi nikamuaga huyu dada, mie ninashuka hapa mama nikapumzike na safari nitaendelea kesho maani kuzika Lushoto ni Alhamisi wewe ni kesho endelea na safari, msomaji wangu kumbuka huku nilipaswa kushuka moshi mjini, Arusha nashuka angalau kujifutafuta niwe nadhifu.
Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?
Kwa hakika huyu binti wa Kichaga safarini anaonesha wazi anasimama katika msatari wa Rais John Pombe Magufuli. Swali ni je Mwanakwetu anasimama katika mstari gani? Jibu lake ni hili Mwanakwetu anasima katika mstari wa huyu binti aliyesafiri naye kwa tabu. Kama abiria huyu mwenye mtoto ametaabika katika barabara hii nzuri inakuwaje kama angepitia njia ya Musoma Serengeti Rusha na Dunda Dunda tele? Abiria anaweza kutapika hadi nyongo na kisha kufariki dunia. Kwa hiyo serikali yetu lazma ipambane na ujenzi wa Barabara hii hizo KM 452 zijengwe yale maeneo ambayo wanyama wanavuka mnaacha na hilo litasaidia kwa mikoa ya Arusha, Manyara Mara, Mwanza, Shinyanga Simiyu na Geita kuongeza uungwaji mkono wa Serikali inayotokana na CCM.
Mwanakwetu anakumbusha pia msomaji wake aangalia huyu binti alivyoteseka safarini na hali yake ya kutapika na namna Mwanakwetu baba wa hiari alivyomsaidia kubeba mtoto, hili linakumbusha kuwa safari yoyote ya Mwanamke au Mwanaume lazima tutegemeane kila mmoja apewe nafasi yake, ni vigumu mwanamke kufanikiwa kwa kutumia nguvu za wanawake peke yake hili gumu lazima utagonjwa mwamba, ukiwa mwanamke wataje sana wanaume, waheshimu wakuunge mkono ili wakuunge mkono, wanawake ongea nao vizuri ukiwaomba wakuunge mkono katika mazingira fulani.
Naye Abdul Mtulya katika makala yake ya Magazeti ya Ujerumani ya Agost 29, 2013 miaka 12 iliyopita alinuku umaelezo ya Wahariri wa Magazeti ya Ujerumani,
“Wahariri hao walikumbushia suala la maadili ya jamii ya Ujerumani kuwa Katiba ya Ujerumani iliyojengwa katika msingi wa haki za binadamu, inawawajibisha Wajerumani kuwa macho juu ya udhalimu wowote ule, usikae kimya katika udhalimu timiza wajibu wako kukataa udhalimu na yoyote anayefumbia macho udhalimu mbele ya picha zinazoonesha raia walidhulumiwa nafsi zao kwa kuuwawa kwa gesi ya sumu anasapwa afunge domo lake, hata hivyo huyu mfunga domo lake pia anapaswa kujihadhari na ushetani wa kulipiza kisasi.”
Hayo pia ndiyo yanayosemwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu haki za binadamu, katiba haitaki wananchi kuwa kimya juu ya udhalimu wowote ule na kama mmoja wetu akachagua kukaa kimya lakini huko kukao kimya kwake isije ikawa chanzo ya ushetani wa kulipiza kisasi, hii pia ni tahadhari ya Mwanakwetu kwa Tanzania katika hali ya siasa za sasa kuekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Katika makala yake ya pili ya Abdul Mtulya
“Wahariri wa magazeti ya Ujerumani walimtaja Chrstian Wulff Rais wa Ujerumani wa zamani ambaye alishitakiwa, wahariri hao walisema Wulff hakufaa kuwa rais wa taifa hilo, hivyo ilikuwa sahhi kwake kujiuzulu, lakini Wahariri hao walisema Wulff kama binadamu pengine tabia yake ilikwenda kombo lakini mabaya yanayazungumziwa dhidi yake na waliokuwa karibu naye yanakwenda mbali mno, haya yanayozungumzwa yanapaswa kuwa darasa kwetu sote.”
Kujiuzulu kwa Rais wa Ujerumani wakati huo ndugu Christian Wulff Mwanakwetu anakulinganisha na kifo cha Rais John Magufuli, maana yake kuwa nje ya madaraka. Wulff kifo cha kisiasa huku Magufuli kifo cha kiwiliwili.Hata kama Rais Magufuli alikuwa mbaya kiasi gani, wapo watu tena wengi ambao hawaamini katika ubaya huo unaosemwa, hawa wasioamini katika ubay wa Magufuli wanasimama katika mstari wa John Pombe Magufuli akiwamo huyu mama safarini. Magufuli kama Christian Wulff wote ni binadamu waliozaliwa na mwanamke, wenye nyama na damu, kikubwa katika hayo mabaya yao yanayosemwa mimi na wewe tunajifunza nini?
Mwisho Mwanakwetu yu njiani anakwenda kumzika Bibi Kolowa nyumbani kwake Lushoto mkoani Tanga, Bibi Kolowa alikuw make wa Dkt Sebastiani Kolowa aliyeiongoza KKKT kwa miaka mingi wakisimamia miradi ya maendeleo ya kiroho na Kimwili
“Hivi mathalani Dkt Sebastian Kolowa akapewa uhai tena, akajaa duniani kuja kumzika mkewe Elfirda, je kiongozi huyu wa kiroho ataikuta Tanzania na nyumbani kwao Bumbuli kumeendelea au Tanzania imerudi nyuma? Kwa uhakika yapo yatakayomvutia lakini binafsi yangu ninaona Baba Askofu Dkt. Sebastian Kolowa atatoa mchozi juu ya baadhi ya matukio ya nduguze mathalani suala la watu wasiojulikana, Watanzania kuuwana wenyewe kwa wenyewe kwa sababu za kijinga.”
Mwanakwetu upo?
Kumbuka,
“Usiwabague Kondoo Kwa Yao Madhaifu. Akija Kumzika Mkewe Atakasirika.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
Post a Comment