BABA ANAMSALIMIA MAMA SAA NGAPI -NYAKABAYA

 




Adeladius Makwega-MWANZA

Jioni ya Juni 23, 2024 wanachuo wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya walifanya Tamasha la Masoko Katika Michezo katika viunga vya chuo hiki, huku msanii wa muziki wa Kisukuma maarufu kama Nyakabaya akitumbuiza. Msanii Nyakabaya katika tamasha hilo aliweza kukonga nyoyo za wananchi wa Malya na viunga vyake ambapo nusu ya uwanja huu wa chuo hiki ukijazwa na watazamaji .”

“Eti jamani eeeh, nauliza wale tunaofanya kazi usiku kama vile walinzi, mambo ya night shift baba anamsalimia mama saa ngapi?”

Mashabiki wa tamasha hilo wakisema mchana naye, Nyakabaya akijibu hapana mashabaki wakasema usiku yakabaya akasema hapana.Nyakabaya aliimba wimbo wenye maudhi hayo lakini jibu halikupatikana. Wakizungumza katika onesho hilo baadhi ya mashabiki walisema;

“Nilisikia tangazo mitaani, mwanzoni nilidhani utani , kumbe ni kweli, nimekuja hapa kuhakikisha kama kweli, nimelipa shilingi 500/mimi na mke wangu sasa nimemuona Nyakabaya na wasanii wenzake wanaokaribia 20, nimefurahi sana.”

Getruda Masanja mkaazi wa Stesheni ya Gari Moshi hapa Malya alisema.Tamasha hilo lilikuwa na kiingilio na zaidi ya mashabiki 1000 waliingia uwanjani ambapo kulizungushwa vizuia mtu kuoa, huku wageni kadhaa kutoka Chuo cha Maedeleo ya Wananchi (FDC) wakiwapo uwanjani.

 

Akizungumza katika tamasha hili Mwenyekiti wa wanachuo walioanda Kasili Lameck ambaye ni Waziri Mstaafu wa Habari wa Serikali ya wanachuo alisema kuwa nia ya tamasha hilo ni kuhakisha yale waliojifunza darasani wanayafanya kwa vitendo na kwa hakika wameyafikia malengo yao.

Mdau mmoja wa sanaa hapa uwanjani Malya ambaye hakutaka jina lake kutajwa, alipiga mahesabu haya,

“Kumualika Nyakabaya katika tamasha moja gharama zake ni kati ya shlingi 1,200,000- 2,000,000/- anaweza kuimba kati ya saa 2-5. Kwa hesabu ya watu waliofika kuona tamasha hili kadilio ni watu 1000 -1200 mara shilingi 500 jumla kuu ni shilingi 500,000/- ukijumlisha gharama zote za maandalizi ni karibu shlingi 3,000,0000/-. Kama wangetaka kupata faida wangepata watazamaji kati ya 3000-5000.”

Ndugu huyu aliendelea kusema kuwa matamasha haya kwa jamii ya Wasukuma  kabla ya kuandaa huwa kunafanyika ushirikina ili kukwepa hasara, haya yanafanyika hata katika harusi zao.Akilijibu hilo Bi Modesta Lupenza ambaye ni miongoni mwa wanachuo walioanda tamasha alisema.

“Imani za kishirikina katika jamii zetu zipo lakini ili kufanikisha mambo lazima lazima kikundi kiwe na mipango madhubuti ya mwongozo wa namna ya kufanya huku wakiwa na mtaji wakiweka kando uzembe.”

Kwa upande wake Ndinagwe Sungura ambaye ni Makamu Rais Serikali ya wanacho Mstaafu yeye alikubalia kwa matamasha haya yanapoandaliwa kuna changamoto tele na ni lazima zitatuliwe kwa wakati bila kulaumiana.


 

Akizngumza katika kuhitimsha hili Ladisilaus Nunguya Mjumbe wa bodi wa MCSD na Rais Mstaafu wa Serikali ya Wanachuo aliipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kukisimamia chuo hiki vizuri huku akisema hapo mbele MCSD kitakuwa chuo chenye mafanikio makubwa.

“Mimi na Wezangu kadhaa sasa tumeiva na tupo tayari katika  kutekeleza majukumu yoyote ya michezo mbeleni. MCSD imetupatia elimu bora na sasa tupo imara.”

Akihitisha tamasha hilo Makamu Mkuu wa Chuo Cha Maendeleo ya Jamii(FDC) ndugu George Lubinza alisema kuwa anawashukuru wanachuo hao kwa kumualika katika tamasha hilo;

“Mahusiano haya yanajenga udugu baina FDC na MCSD na kwa siku ya leo na mimi nimejifunza mengi na jamii ya Malya inanufahika na matamasha haya.”

Mwishoni wa tamasha hilo Bi Consolata Mkwakwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa wanachuo hao aliwashukuru wanadarasa hilo na kuomba wabaki kuwa wamoja milele,

“Jamani maisha yanaendelea umoja ni nguvu…kidole kimoja hakivunji chawa.”

Msomaji wangu kumbuka,

“Baba Anamsalimia Mama Saa Ngapi?”

makwadeladius@gmail.com

0717649257





 

0/Post a Comment/Comments