Adeladius
Makwega-MWANZA
Maisha
baina ya jamii ya Wasukuma na jamii za Pwani yana simulizi ndefu ambazo hata
kama zikiandikwa na kusimuliwa zinaweza zisiishe, japokuwa simulizi chache mno
zimeandikwa.
Mwanakwetu
leo anakuomba msomaji wake kwa heshima na taadhima zote akusimulie simulizi
mojawapo ambayo iliandikwa mwaka 1970 na ndugu S. Kazi ambaye alifanya utafiti
juu ya maisha baina ya Wasukuma na na makabila ya Pwani .
Ndugu
S Kazi anabainisha kuwa mawasiliano baina ya Pwani na Bara ni ya miaka mingi, huku
yakipitia hatua mbalimbali, tangu kutembea umbali mrefu kwa miguu na kutumia wanyama
kama punda ambapo safari hizo zilitumia miezi mingi hadi Wasukuma kufika Pwani
ya Bahari ya Hindi.
Hali
ya usafiri ilikuwa ya nafuu baada ya Mjerumani kujenga reli ya kati ambapo usafiri
wake ulikuwa mwepesi na wakati huohuo kulikuwa na ujio wa motakali(magari ya
mota).
S
Kazi anasema kuwa watumishi wengi katika gari moshi na vituo vyake vilivyotapaka
tangu Pwani hadi Bara walikuwa makabila ya Pwani wakiwamo Wazaramo , Wakwere , Waruguru,
Wapogoro, Wandengeroko na mengine.
Mjerumani
aliwahusudu hawa jamaa kwa sababu kadhaa ikiwamo ujanjaujanja, kufahamu lugha
nyingi na pia kuwa wajuzi wa Kiswahili.
Msomaji
wangu leo Mwanakwetu hataki kuzungumzia mahusiano baina ya Wasukuma na makabila
ya Pwani wakati wa Wakoloni bali anazungumzia kabla ya ugeni huo.
Ndugu
S Kazi anasema kuwa siku moja Wasukuma walikwenda Pwani wakauza walivyobeba na
kununua walivyovitaka , wakaifunga mizigo yao wakijianda kurudi Usukumani.
Wakati
wanataka kurudi kwao Bara, Wazaramo walimpa zawadi mkuu wa msafara wa Wasukuma
na zawadi hiyo ilikuwa ni mzigo wa NAZI kavu zilizokwisha fuliwa. Walipouliza zawadi
hii inatumikaje Wazaramo walimpa maelekezo yao msaidizi wa mkuu wa msafara wa
Wasukuma,
Walipofika
mzigo huo wa NAZI ulifunguliwa na wale waliambatana na Mkuu wa Msafara
wakagawawiwa kila mmoja NAZI mbili mbili ili wakatazitumie majumbani mwao.
Msaidizi
wa Mkuu Msafara huo aliyepewa maelekezo na Wazaramao ya namna ya kuitumia NAZI
hizo aliwaambie wenzake,
“Unachotakiwa
kufanya ni kukoka moto, unauwasha, unauweka chungu chenye maji mekoni na unaiweka
nazi hiyo katika chungu chenye maji kama ilivyo, Nazi itachemka kwa muda mrefu
hadi itaiva na NAZI itakuwa tayari kuliwa kama KIAZI, ni tamu sana.”
Wale wote waliotoka safari ya Pwani waliyapokea
maelekezo hayo na kurudi majumbani mwao na kuwapa maelekezo hayo wake zao na
shughuli yakuipika NAZI ilianza.
Kumbuka msomaji wangu katika mila za Kiafrika zawadi
huwa inakuwa ni kitu cha kwanza kufunguliwa na kuliwa, kwa hiyo kila aliyepewa zawadi ya NAZI
alipofika nyumbani kwake kuipika NAZI lilikuwa jambp la kwanza.
Wanawake wa Kisukuma walipokea maelekezo ya kupika
NAZI vizuri, pika pika na wewe ya NAZI ikaanza
, akina mama wa Kisukuma kila walipobonyeza NAZI hiyo ilikuwa bado ngumu, waliongeza
maji na kuweka magadi NAZI bado ilikuwa ngumu, kuni zilichochowa weee mapishi
yaliendelea ili waweze kula zawadi hiyo kutoka Uzaramoni lakini wapi NAZI hakuiva
.
Wanawake wa Kisukuma kuwaambia waume zao NAZI
haiivi kwanza ilikuwa aibu, maana huko ni kushindwa kutekeleza majukumu yao
kama wanawake.
Akina mama wa Kisukuma kwanza waliulizana wao
kwa wao majibu hayakupatikana hata mmoja NAZI hiyo kuiva. Hapo ndipo jambo hilo
lilikwenda kwa waume zao.
Wasukuma wakatambua kuwa Wazaramo wamewachezea
mchezo, hapo tayari Wazaramo walikuwa wameshawazidi kete Wasukuma. Wasukuma walikasirika
mno lakini safari ya kutoka Bara hadi Pwani ni ndefu sana njiani hasira
zinaweza kukuishia, lakini Wasukuma wakawa wanajipanga namna ya kulipiza
kisasi.
Mwanakwetu siku ya leo anasema nini ?
Unaweza ukapewa zawadi vizuri tu na ukaifurahi
mno hiyo zawadi, hoja si kupewa zawadi bali la msingi ni yale maelekezo yanayotolewa
je yatakuwa sahihi? Unaweza kupewa kitu cha thamani kubwa lakini maelekezo
yakewa siyo sahihi na kile kitu cha thamani kisiwe na manufaa kwako hata kidogo.
Mwanakwetu upo?
Nakutakia Siku Njema
0717649257
Post a Comment