Adeladius Makwega-Mwisenge.
“Leo Tunasherehekea sikukuu kuu ya Pentekoste. Msimu wa Pasaka unafikia kilele chake katika kushuka kwa Roho Mtakatifu, utimilifu wa ahadi ya Yesu kwa wanafunzi wake.Injili inaturudisha kwenye Jumapili ya Pasaka, wakati Bwana aliyefufuka alipowatembelea wanafunzi wake, waliokuwa wamejificha nyuma ya milango iliyofungwa ya chumba cha juu. Hapo Yesu aliwapa zawadi yake ya amani, akawavuvia Roho Mtakatifu ili kupitia wao, wengine pia wapate kupokea msamaha.
Sikukuu ya leo somo la kwanza kutoka kitabu cha Matendo ya Mitume linatoa simulizi ya Mtakatifu Luka kuhusu kilichotokea siku ya Pentekoste. Walikuwa wote wamekusanyika katika nyumba moja, ghafla pakasikika sauti kama ya upepo mkali uliovuma na kuijaza nyumba yote. Ndipo ndimi kama za moto zikaonekana na kutua juu ya kila mmoja wao. Roho Mtakatifu akawawezesha kutangaza Habari Njema kwa lugha mbalimbali, na kila mtu aliwaelewa.
Hili ndilo leo tunalolihitaji sana, ndugu zangu, tunaomba ili Roho Mtakatifu aje kwetu na kutupulizia upepo wake, atuongoze kuelekea katika amani na kufikia msamaha, na pia kujaliwa kutambua vipaji mbalimbali kwa wenzetu, kuelekea umoja na mshikamano.
Njoo Roho Mtakatifu, njoo.”
Haya ni maelezo machache ya ufunguo wa mahubiri ya Kadinali Luis Antonie Tagle Mkuu wa Propaganda Fide ya Kanisa Katoliki inayoshughulika na Uinjilishaji wa watu Ulimwenguni.Haya ni Vatikani nako katika Parokia ya Mwisenge Jimbo Katoliki la Musoma wakati wa mahubiri ulisomwa waraka mmoja mrefu kutoka kwa viongozi wa walei Wakatoliki Tanzania, huku ukizijenga kila aya zake na rejea ya nukuu katika Biblia.
Baadaye Wakatukumeni kadhaa walibatizwa na waamini wote wakirejea ahadi ya ubatizo.
Kutokana na Sherehe ya Pentekosti Mwanakwetu amekuandalia utenzi huu msomaji wake.
Leo twasherehekea, Pentekoste adhimu,
Roho ashuka kwa nguvu, zawadi ya Karimu,
Ahadi ya Yesu yatimia, kwa wafuasi wake wote,
Pasaka yafika mwisho, kwa neema ya adhimu.
Injili yatukumbusha, siku ile ya furaha,
Bwana afufuka kweli, akawapa wao raha,
Milango ikiwa imefungwa, kwa hofu na mashaka,
Amani awavuvia, Roho awapa baraka.
Matendo yatueleza, Luka atoa habari,
Walipokusanyika wote, kwa moyo wa subiri,
Upepo wavuma kwa nguvu, ukajaza mahali,
Ndimi za moto zatua, lugha nyingi Zikasikika
Leo nasi twaomba, ndugu kwa moyo mmoja,
Roho aje atujalie, neema tele na haja,
Atuongoze kwa amani, na msamaha kwa pamoja,
Njoo Roho Mtakatifu, njoo utupe mwangaza.
Wakati haya ni ya ndani ya kuta za Kanisa na Sikukuu ya Pentekoste hali ya hewa ya Mji wa Musoma ni ya joto kati ya nyuzi joto 21 na 28, unyevunyevu ni wa asilimia 0, ujirani na mvua ni wa asilimia 51 huku upepo ukivuma kwa KM 13 kwa saa.
Mwanakwetu upo ?Kumbuka
“Roho Mtakatifu Atuelekeze Kutambua Vipaji Mbalimbali kwa Wenzetu.”
Nakutakia Siku Njema.
0717649257
.gif)
.gif)








Post a Comment