Chuo cha DMTA Jawabu la Uchumi wa Bluu

 








Adeladius Makwega–Mwanza

Mwanakwetu kwa muda mrefu amekuwa na kiu kubwa ya kufahamu kwa kina juu ya mafunzo ya Ubaharia nchini Tanzania, kila mara amekuwa na maswali mengi juu taaluma hii na kila akiona meli iwe ziwani au baharini maswali lukuki yamekuwa yakimjia.

Mungu bahati baadaye alijulishwa juu ya Dar es Salaam Maritime Training Academy(Chuo cha DMTA) chuo pekee cha Ubaharia cha binafsi nchini Tanzania, hivyo basi alitoka zake Musoma hadi Mwanza na kisha Mwanza hadi Dar es Salaam ili aweze kuona kwa macho yake, kujua zaidi juu ya taasisi hii binafsi inayotoa mafunzo haya ya ubaharia nchini .

Mwanakwetu mwenye kiu na kufahamu elimu ya ubaharia hapa alifika Mtaa wa Uhuru / Clock Tower Plot # 2035 Block 155, Jengo la NHC, Ghorofa ya 3 Chumba 304 na kisha Ghorofa ya 4 Chumba 404.

Mwanakwetu bila hiyana alipokelewa na uongozi wa taasisi hii binafsi vizuri ambayo inayotoa elimu ya ngazi ya Astashahada ya Ubaharia na hapa akaanza kupewa maelezo kwa ukarimu tele hatua kwa hatua. Huku injinia Lameck Sondo ambaye ni miongoni mwa viongozi wa taasisi akiwa mwenyeji wake:

“Kwanza pole kwa safari, pia karibu sana Chuo cha DMTA, hapa tunawafunzi kutoka mataifa kadhaa na mikoa yote ya Tanzania wakiwamo wanafunzi saba kutoka Kanda ya Ziwa, taasisi yetu imejikita katika kuunda mustakabali wa wataalamu wa baharini kupitia mafunzo ya kiwango cha kimataifa, ujifunzaji wa vitendo, na utaalamu unaoongozwa na mahitaji ya sekta hii. Kwa kujitolea kwa dhati katika usalama, ubora, na weledi, tunatoa mafunzo muhimu kwa wanaotamani kuwa mabaharia, wakihakikishiwa wanapata ujuzi na maarifa yanayohitajika kufanikiwa katika sekta ya ubaharia kitaifa na kimataifa.”

Injinia Sondo pia aligusia mafunzo yanatolewa ikiwa ni pamoja na Huduma ya Kwanza ya Msingi, hapa alisema wanachuo wote wanajifunza mbinu za msingi za huduma ya kwanza zilizoundwa kwa mazingira ya baharini, kuhakikisha watu wanaweza kutoa msaada wa haraka wakati wa dharura.

 

Wanawake wa Chuo cha DMTA hawakumtenga Mwanakwetu walimpokea kwa mikono miwili miongoni mwao ni Bi. Dorine Songoro ambaye ni msajiri wa Chuo cha DMTA yeye alisema kwa sasa ubaharia unalipa maana yule baharia wa ngazi ya chini kabisa melini analipwa dola 450 ambayo ni pesa inaweza kumsaiadia kijana wa Kitanzania kuishi na kwa upande wake Injinia Sondo aliongeza kuwa:

“Mbinu za Kujinusuru huwapatia wanafunzi wetu ujuzi na mbinu muhimu za kuishi katika hali za dharura baharini.”

Mwanakwetu akiwa anaelekea ghorofa ya nne ya Chuo cha DMTA kwanza ilisikika sauti ya honi ya meli poooooo…! Injinia Sondo alijibu kuwa hiyo ni meli inaingia bandarini na kwa mbali aliomuoneshwa Mwanakwetu Bahari ya Hindi na meli zikiingia, zingine zikitoa nanga. Hili lilimthibitishia Mwanakwetu kuwa haya ni mazingira mazuri na sahihi ya kujifunza ubaharia.

Mwanakwetu akasema atamleta mwanaye asome taasisi hii ili na yeye awe binadamu katika watu. Bi Dorine Songoro akacheka akasema kijana wako ni binadamu tayari, hapa akija tutampa mbinu na ujuzi wa ubaharia ili aweze kuifanya kazi hii kwa ufanisi, karibu sana Chuo cha DMTA. Bi Songoro akaongeza:

“Unaona wanafunzi wa ubaharia wakiwa wanajifunza?”

Mwanakwetu alijibu ndiyo. Bi Songoro aliyataja mafunzo mengine ya Chuo cha DMTA ikiwa ni pamoja na Kuzuia na Kupambana na Moto, akisema kuwa hapa wanachuo wao wanapewa mbinu za kuzuia, kudhibiti, na kupambana na moto ndani ya vyombo vya majini, kuhakikisha hatua za usalama zinaeleweka na kutekelezwa ipasavyo.

 

Bi Songoro akimalizia kuyataja mafunzo mengine alisema ni pamoja na Usalama Binafsi na Uwajibikaji wa Kijamii, hapa shabaha kinachosisitizwa ni umuhimu wa usalama binafsi na tabia ya kuwajibika wakiwa kazini, ikikuza utamaduni wa usalama na uwajibikaji. Sambamba na haya aliongeza kuwa Sekta ya ubaharia ina mchango mkubwa na thabiti katika uchumi wa Tanzania kupitia Uchumi wa Bluu, usafirishaji wa mizigo, na ufunguaji wa fursa za ajira. Kazi ya ubaharia ni chanzo muhimu cha mapato ya kigeni kwa nchi nyingi.

“Sisi kama Chuo DMTA tunaunga mkono juhudi za kupanua wigo wa utoaji mafunzo ya kiwango cha kimataifa ili kuwawezesha vijana wengi wa kike na wakiume kuajiriwa katika meli za kitaifa na hata za kimataifa. Huku kwa sasa Watanzania wamewekeza zaidi katika kuimarisha mafunzo ya uchumi wa bluu na uweledi wa mabaharia kama tulivyoanzisha Chuo cha DMTA.”

Baadaye Bi Dorine Songoro aliyataja mawasiliano yao:

“Kwa simu namba +255 765 616 129 / +255 766 288 288., Barua Pepe info@dmta.ac.tz na Anwani na S. L. P. 3625, Dar es Salaam, Tanzania.”

Msomaji wangu Mwanakwetu yupo Chuo cha DMTA na kwa hakika Chuo cha DMTA siyo wachoyo namba moja kati ya hizo ukipiga unampata Bi Dorine Songoro moja kwa moja. Maswali yote juu ya Chuo cha DMTA na ubaharia utapatiwa majibu, huku maswali mengine Mwanakwetu anasema hapana kuuliza.

 

Mwanakwetu baada ya kumaliza mazungumzo haya na Injinia Lameck Sondo na Bi Dorine Songoro aliangalia mandhari katika mazingira ya taasisi hii huku akijifunza namna yalivyo tangu vyumba vya madarasa, maktaba, kumbi na eneo lote na kujifunzia huku yakiwa mazinginra ya kuvutia kwa elimu hii ya ubahari hapa nchini. Mwanakwetu baadaye aliagana nao na kisha kuanza kutoka Dar es Salaam kurudi Mwanza na kuelekea Musoma na akiwa njiani akaamua kukutayarishia makala haya kama yalivyo

Mwanakwetu anasema nini siku ya leo?

Kwa hakika hii ni safari ya Mwanakwetu katika Chuo Cha DMTA na ameona asikae nayo moyoni, bali akusimulie kama ilivyo, ikiwa ya motomoto, shabaha ni kwako wewe kijana, mzazi au mlezi kuchangamkia fursa ya kujifunza ubahari maana kizuri kula na mwenzako, fursa zipo waziwazi, tembelea taasisi hii, tembelea tovuti yao , haya yakikushinda piga simu yao kujifunza kwa kina ili kuchangamkia fursa kedekede za ubaharia.

Rejea maelezo ya Bi Dorine Songoro

“Ukipata kazi ya ubaharia unalipwa kwa fedha za kigeni na hivyo ni kukuza uchumi wa bluu wa taifa lako.”

Mwanakwetu Upo? Kumbuka

“Chuo Cha DMTA Jawabu La Uchumu wa Bluu”

Nakutaki siku Njema.

makwadeladius @gmail.com

0717640257.











 

 

 

0/Post a Comment/Comments