Adeladius Makwega-MWANZA
Katika matini iliyotangulia Mwanakwetu alieleza namna utani wa WAPARE ulivyotokea huku nikitaja hata jina la kabila hili la asili na namna jina jipya lilivyotokea.
Ndugu S. Mesaki katika utafiti wake juu ya Utani wa Wapare anasema kuwa kama MBANGA akifariki ambaye ni ukoo watawala mwenye wajibu wa kuchukua mifupa na fuvu la marehemu na kulipeleka katika msitu wa WACHONVU. Mchonvu akifanya kazi hiyo kama maziko ndiyo kusema wao walikuwa na utaratibu kuwa mwili huo ulikuwa ukihifadhi hadi uharibike alafu mifupa ndiyo inayopelekwa msituni kama maziko.
“MCHONVU huyu akishamaliza kazi hiyo
alikuwa akilipwa mbuzi au fahari ( dume kubwa la ng’ombe) wanyam hao walitolewa
kama ujira kwa kazi hiyo. Mara akishalipwa huwa anasema maeneo kuwa mbona hafi
MBANGA mwinngine ili apate dume la ng’ombe lingine? ”
Pia panapotokea msiba mtani hupewa
kazi ya kugawa mali za marehemu kwani yeye huwa hana aibu na anaweza kusema
maneno kama haya.
“Ghuna icho ambu nich meirihirwe
akinafwe.”
Akimaanisha kuwa chukua hiyo kwa
kuwa una furaha kwa kuwa amefaki. Maneno hayo yakiambatana na mgao wa nguo au
mali zingine za marehemu. Mtani hawezi kuishia hapo bali anaweza kusema maneno
haya:
“Mie senafwa se nani erundie.”
Hapa akimaanisha kuwa yeye hawezi
kufa kama alivyokufa mtani wake, anafanya hivyo hiyo akijilinganisha na kifo
cha marehemu ambaye anatoka kwa watani wake.
“Ula mghoma wafwa.”
Akimaanisha yule ng’ombe mkongwe
amefariki akimlinganisha marehemu ambaye alikuwa mzee na ng’ombe.
Pia mtani anaweza kwenda mbali
kabisa kwa kusema:
“Kama wala kiteta.”
Hapa akimaanisha kuwa kama ndugu wa
marehemu wameshamla nyama marehemu huyo.
Utani unaonekana katika mazishi
ambapo kaburi likiwa limeshachimbwa na mwili wa marehemu upo unataka
kuzikwa basi mtani anaweza kuingia ndani ya kaburi na kusema hatoki hadi apewe
mbuzi. Hilo kweli hufanyika na mtani hupewa mbuzi alafu mazishi hufanyika.
Wapare ni kabila lililokuwa
linafanya tohara kwa wavulana na wasichana kabla ya sheria kukataza tohara ya
wasichana. Wakati shughuli hiyo kulikuwa na aina ya utani ambayo ilikuwa
inafanywa hasa wale wazazi waliotahiri watoto wao awali na wale wanaofanyiwa
tohara kwa siku hiyo.Utani huo ulikuwa unafanywa kwa nia kama ya kuwapongeza
kwa watoto hao kwa kufikia hatua hiyo ya utu uzima na kueleza umuhimu wa
shughuli hiyo kwa kabila hilo.
Utani huo ulikuwa ni wa wazazi kwa
wazazi tu. Kwa wale waliofanyiwa tohara ilikuwa ni pongezi.Utani katika
shughuli hiyo uliendana na nyimbo huku pongezi zikitolewa.
“Idhihira, waehija, eee, wenyongie
ukabanda, eee…iki nimuenda mbora wako…”
Wakimaanisha kuwa ulikuwa mwembamba
lakini sasa umekuwa mnene.Maana yake baada ya kufanyiwa tohara hiyo sasa
umekuwa mkubwa na umenawili.
Mwanakwetu anaomba aiishie hapo kwa
leo.
Je kipi kitafuta ? Subiri
matini ijayo.
0717649257
Post a Comment